Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA WASIWASI(ANXIETY DISORDER)

 WASIWASI

• • • • •

UGONJWA WA WASIWASI(ANXIETY DISORDER)


Katika maisha ya binadamu, kuna vitu vingi huweza kusababisha hali ya hofu pamoja na wasi wasi Kama vile; Mtu wako wa karibu akiugua sana, kuishiwa na fedha huku kuna mahitaji ya Lazima, Wakati unafanya interview kwa ajili ya kuajiriwa sehemu flani, na kwa wanafunzi hupatwa sana na hii hali ya hofu na wasiwasi hasa kipindi cha Mitihani, Pamoja na sababu zingine ambazo zijazitaja.


Lakini fahamu kwamba, Wasiwasi huu unaweza kuwa Ugonjwa bila wewe kufahamu kwamba una Ugonjwa wa wasiwasi au kwa kitaalam hujulikana kama Anxiety Disorder.Je utajuaje kama wasiwasi na hofu uliyo nayo ni Ugonjwa?


HIZI HAPA NI DALILI ZA UGONJWA WA WASIWASI(ANXIETY DISORDER)


1. Wasiwasi ambao huambatana na  kukamaaa kwa misuli ya mwili


2. Wasiwasi ambao huambatana na maumivu makali ya kichwa


3. Wasiwasi ambao huambatana na mwili kuchoka sana pamoja na kuishiwa nguvu ya kufanya chochote


4. Wasiwasi ambao huambatana na kukosa usingizi kabsa,wengine wanaweza kukaa hata wiki Nzima hawalali


5. Wasiwasi ambao huambatana na kupoteza kumbukumbu kabsa


6. Wasiwasi ambao huambatana na kuwa na hasra za haraka,kitu kidogo tu mtu kakasirika kupita maelezo


7. Wasiwasi ambao huambatana na kushindwa kufanya vitu katika hali ya utulivu


8. Wasiwasi ambao huambatana na kufanya vitu kwa haraka, na wengine hata kushindwa kujieleza kabsa kwanini wamefanya maamuzi ya jambo flani kama walivyofanya.


CHANZO


Hata hivo Ugonjwa huu huweza kuhusishwa na vyanzo mbali mbali kama,


– Mabadiliko ya gafla ya vichocheo vya mwili


– Hali ya kimazingira  ambayo mtu amekutana nayo


– Msongo wa Mawazo 


– N.K


Kwa Mtu mwenye hali hii ni lazima apate msaada wa haraka kuepuka madhara makubwa ambayo huweza kujitokeza kutokana na Tatizo hili, Kama vile;


* Kupoteza uwezo wa kufanya kazi kabsa

* kupoteza ajira kama ni muajiriwa

* kupoteza kumbukumbu

* Kujiua au kudhuru wengine


BAADHI YA MAMBO YA KUFANYA KUKUSAIDIA UKIWA KATIKA HALI HII


• Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara kila siku


• Jitahidi kujichanganya na watu usikae peke yako Ndani


• Hudhuria sehemu za Ibada kama Kanisani au Msikitini


• Epuka hali yoyote inayokuletea msongo wa mawazo


• Sikiliza Mziki au nyimbo mbali mbali za kukuburudisha sio za kukupa huzuni


• Kama wewe ni mpenzi wa movie,angalia movie unazozipenda


• Pata Mda wa kutosha wa kulala



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.