Antibiotics hutibu maambukizi yanayosababishwa na Bacteria Pekee na Wala haziwezi kutibu Viruses
Antibiotics hutibu maambukizi yanayosababishwa na Bacteria Pekee na Wala haziwezi kutibu Viruses
Tumia Dawa Jamii ya Antibiotics kwa Usahihi wake, Dawa hizi hutibu tu baadhi ya maambukizi ambayo husababishwa na Bacteria kama vile;
– UTI,Strep throat,Whooping Cough n.k
Ila antibiotics haziwezi kufanya kazi kutibu maambukizi ambayo husababishwa na Viruses kama vile;
– Flu,Covid-19,Masundo sundo(genital warts) n.k
Matumizi ya Antibiotics sehemu ambapo hazihitajiki badala ya kukuletea faida huweza kukusababishia madhara,
Mwili wako unaweza kuonyesha matokeo mbali mbali kama umetumia dawa hizi isivyosahihi, kama vile;
• Kuanza Kupata vipele au rashes kwenye ngozi yako
• Mwili wako kuanza kuwasha sana
• Mtu kuhisi kichefuchefu na kutapika
• Mtu kupata kizunguzungu kikali
• Mtu kuharisha
• Mtu kupata maumivu ya tumbo n.k
USHAURI:
1. Sio kila Ugonjwa hutibiwa kwa Dawa Jamii ya antibiotics,hivo ongea na wataalam wa afya kwanza,upewe ushauri juu ya dawa sahihi kwako
2. Epuka kuzidisha kiwango cha Dawa Ulizoandikiwa eti ili upone kwa Haraka zaidi
3. Ukiona unapata reactions zozote baada ya kutumia dawa,unaweza kuuliza kujua ni sahihi au kuna kitu hakipo sawa.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.