Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Homa ya Mafua Flu(influenza) chanzo,Dalili na Tiba yake

Homa ya Mafua Flu(influenza) chanzo,Dalili na Tiba yake

Homa ya mafua,Flu(influenza) ni maambukizi ya viruses ambao hushambulia puani,kwenye koo, na mapafu ambavyo hivi ni sehemu ya mfumo wa hewa(respiratory system).

Baadi ya watu hupona wenyewe, ila wengine hupata madhara zaidi hata kuweza kusababisha vifo kwa baadhi ya watu hasa kwa Nchi za Wenzetu kama vile Marekani n.k

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA MADHARA MAKUBWA YANAYOTOKANA NA HOMA YA MAFUA(FLU/INFLUENZA)

– American Indians au Alaska Natives

– Watoto wenye umri wa chini ya Miaka 2

– Watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 65

– Wanawake wajawazito kipindi cha Homa ya mafua(Flu season)

– Watu wenye Kinga dhaifu kama wagonjwa wa UKIMWI

– watu wenye magonjwa ya kudumu kama vile;

• asthma,

• magonjwa ya moyo(heart disease),

• magonjwa ya Figo(kidney disease),

• Magonjwa ya Ini(liver disease)

• Ugonjwa wa Kisukari(diabetes) n.k

– Watu wenye Uzito Mkubwa Zaidi kuanzia body mass index (BMI) ya 40 au Zaidi.

DALILI ZA HOMA YA MAFUA(FLU) NI PAMOJA NA;

– Kwa mara ya kwanza, Homa ya mafua huweza kuja na Chafya,kuhisi vidonda kooni(Sore throat), au Kuvimba Pua(runny nose)

– Mtu kupata Homa

– Mtu kupata maumivu ya Misuli

– Mwili kutetemeka na kutoa sana jasho

– Kupata maumivu makali ya Kichwa

– Mtu kupata kikohozi kikavu

– Mwili kuchoka kupita kiasi

– Kupata maumivu ya macho

– Kutapika pamoja na Kuharisha, na hii hutokea zaidi kwa watoto n.k

DALILI HIZI HUWEZA KUWA MBAYA ZAIDI, HIVO WAHI HOSPITALINI

• Mtu kupata shida ya kupumua au kukosa pumzi

• Kupata maumivu ya kifua

• Kupata kizunguzungu ambacho ni endelevu

• Misuli ya mwili kuwa dhaifu kupita kiasi

• Kwa watoto:Rangi ya ngozi kubadilika na kuwa blue au kijivu, kwenye Lips za mdomo, kwenye kucha eneo la Nail beds,

• Kupata dalili zote za Maji ya mwili kupungua(dehydration),

CHANZO CHA HOMA YA MAFUA(FLU)

Chanzo cha Ugonjwa huu ni viruses vinavyojulikana kama Influenza viruses,

ambapo unaweza kuvipata kupitia kuruka hewani(air in droplets) kutoka kwa mtu mwingine anayekohoa,kupiga chafya,kuongea n.k

Pia unaweza kuwachukua viruses hawa wakati ukishika vitu vyenye viruses hawa kama vile Simu,computer, n.k, kisha ukawaingiza kupitia machoni,Puani au mdomoni.

MATIBABU YA HOMA YA MAFUA(FLU)

Hakuna tiba zaidi ya Kunywa maji mengi, kupata muda wa kupumzika, na kudhibiti dalili zozote mbaya ambazo huweza kutokea,

Dawa mbali mbali jamii ya antiviral medication huweza kutumika kama vile; oseltamivir (Tamiflu), zanamivir (Relenza), peramivir (Rapivab) or baloxavir (Xofluza). N.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.