Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Usivae Condom kama Mwenzako tayari Kavaa,epuka matumizi ya condom mbili au zaidi kwa wakati Mmoja

Usivae Condom kama Mwenzako tayari Kavaa,epuka matumizi ya condom mbili au zaidi kwa wakati Mmoja,

Condom huweza kutumika kama Kinga ya Kuzuia Mwanamke asibebe Mimba, lakini pia kama kinga dhidi ya magonjwa mbali mbali ya Zinaa,

Ila vyote hivi hufanikiwa kama Ukitumia Condom kwa Usahihi wake.

Watu wengi hutumia condom isivyo sahihi hali ambayo hupelekea hatari Ya Mwanamke Kubeba Mimba, na hatari ya kupata magonjwa ya Zinaa kwa Mwanaume na Mwanamke,

ZINGITIA HAYA ILI CONDOM IWE MSAADA KWAKO;

– Usivae Condom kama Mwenzako tayari Kavaa, mnashauriwa kuvaa condom Mmoja wenu wakati wa tendo,

Na sio wote kuvaa condom kwa wakati mmoja wakati wa tendo la ndoa

– epuka matumizi ya condom mbili au zaidi kwa wakati Mmoja,

Hali ya kuvaa condom mbili au zaidi huweza kusababisha msuguano wakati wa tendo,

Na kisha kuifanya condom kuwa dhaifu zaidi, Hali ambayo huweza kupelekea condom kupasuka.

– Fata Kanuni zote za matumizi sahihi ya Condom kama vile;

Kuepuka mambo haya

1. Kutumia condom moja zaidi ya mara moja( condom reuse)

2. Kutumia condom mbili au zaidi ya mbili kwa wakati mmoja

3. Kutumia condom bila kuacha nafasi kidogo sehemu ya mbele

4. Kutumia condom bila kutoa hewa

5. Kutumia kilainishi kingine chochote kama mafuta n.k kwenye condom

6. Kutumia condom huku ikiwa bado imejikunja

7. Kufungua condom na kuiacha wazi kwa muda,ndipo baadae uitumie

8. Kuchana kifuko cha condom bila kuisogeza,hali ambayo huweza kusababisha kuchana kondom au kuitoboa

N.K

Angali vizuri na chunguza unaweza kuona alama kwa pembeni ya kukuonyesha sehemu ya kuchana kwani baadhi ya condom zina alama ambayo huonyesha kabsa sehemu ya kuchana.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.