Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

FAHAMU KUHUSIANA NA KUWASHWA KWA SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAMKE

FAHAMU KUHUSIANA NA KUWASHWA KWA SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAMKE

Takriban asilimia 10 ya wagonjwa ambao huudhuria kliniki ya kina mama huwa na tatizo hili.

Kuwashwa huku huwa zaidi wakati wa usiku kutokana na kutulia kwa akili, kuchoka kwa mfumo wa fahamu joto na kukosekana kwa hewa maeneo hayo.

SABABU AU CHANZO CHA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

1. Majimaji au uchafu kutoka ukeni usababishwao na trichomonas vaginalis au fangasi

2. Michubuko sehemu za siri

3. Maambukizi
-virusi kama herpes genitalis na vinyama sehemu za siri
-minyoo
-kisonono

4. Allergy- kuvaa nguo za ndani zenye nylon au kufua nguo hizo kwa sabuni yenye kemikali, condom na madawa

5. Kisukari- hupelekea mabadiliko ktk ngozi inayopelekea muwasho lakin pia mabadiliko hayo huchochea fangasi kuota

6. Upungufu wa madini chuma, folic acid, na vitamini A na B 12

7. Matatizo ya kisaikolojia

8. Magonjwa ya tezi ya thyroid

9. Tatizo la Saratani

UTAFITI/UCHUNGUZI
Damu, uchafu kutoka sehemu za siri, mkojo na choo hupimwa ili kutafuta chanzo cha tatizo na kwa baadhi kinyama hutolewa ili kupimwa.

MATIBABU YA TATIZO HILI

1. Usafi wa eneo husika yaani good hygiene

2. Kutumia nguo za ndani zisizobana na ni vyema kutumia zinazotengemezwa kwa kutumia pamba ili kiruhusu hewa kupita

3. Dawa za kuuwa vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile bacteria,fangasi au Virusi lakini pia dawa zenye mchanganyiko wa homoni

4. Kutibu sababu au tatizo husika

5. Upasuaji iwapo uchunguzi utaonesha saratani

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.