Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UMUHIMU WA MAMA KUMNYONYESHA MTOTO

MTOTO KUNYONYA

• • • • • •

UMUHIMU WA MAMA KUMNYONYESHA MTOTO


 1: Maziwa ya mama pekee ni chakula na kinywaji tosha kabisa kwa mtoto mchanga katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya maisha yake. Hakihitajiki chakula wala kinywaji cha aina yoyote, hata maji, katika kipindi hicho.


2:  Kina mama waliojifungua wapewe watoto wao wachanga wawashike mara tu baada ya kujifungua. Washike watoto wao wachanga wakiwa bila nguo ya juu ili ngozi zao zigusane na waanze kunyonyesha ndani ya saa moja baada ya kujifungua.


3: Karibu kila mama anaweza kunyonyesha vizuri. Kunyonyesha mtoto mara kwa mara husababisha kuongezaka kwa maziwa ya mama.


 4: Kunyonyesha husaidia kuwakinga watoto wachanga dhidi ya magonjwa hatari. Aidha hujenga mahusiano ya hisia baina ya mtoto na mama yake.


5:  Endapo mama ana maambukizo ya VVU, aanze (kama hajaanza bado) au aendelee kutumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi na amnyonyeshe mtoto wake maziwa ya mama pekee kwa miezi 6, halafu amwanzishie vyakula vya kulikiza na kuendelea kumnyonyesha hadi atakapotimiza umri wa miaka miwili au zaidi.


6: Mama anayefanya kazi mbali na nyumbani kwake anaweza kuendelea kumnyonyesha mtoto wake. Amnyonyeshe mtoto mara kwa mara pale anapokuwa naye na akamue maziwa yake na kuyahifadhi mahali safi na salama ili mlezi wa mtoto aweze kumnywesha mtoto katika mazigira safi na salama wakati mama akiwa kazini.


7:  Baada ya miezi 6, pale mtoto atakapoanza kula vyakula, unyonyeshaji uendelee hadi mtoto afikishe umri wa miaka miwili na zaidi kwani maziwa ya mama ni chanzo muhimu cha lishe, nguvu na kinga dhidi ya magonjwa.






Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.