Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mwanaume mwenye Umri wa Miaka 40,Na Ugonjwa wa pneumothorax

Mwanaume mwenye Umri wa Miaka 40,Na Ugonjwa wa pneumothorax,

Tatizo la Pneumothorax huhusisha uwepo wa hewa au gesi ndani ya cavity katikati ya mapafu na ukuta wa kifua, hali ambayo huweza kusababisha shida ya Lung collapse.

Mwanaume huyu mwenye Umri wa Miaka 40 alikuwa na Historia ya;

Uvutaji wa Sigara kwa Muda mrefu, na alipelekwa emergency department wiki mbili zilizopita akiwa na shida ya;

• kukohoa sana

• Kupata shida sana ya Kupumua

• Kutokwa na Jasho sana wakati wa Usku

• Kupata maumivu makali ya Kifua hasa Upande wa Kushoto wa Kifua

• Na Pia baada ya kufanyiwa Physical examination ilibainika kwamba,kuna upungufu wa breath sounds kwenye pafu lake la Kushoto

Baada ya Kipimo cha chest radiograph, kilionyesha kwamba ana tatizo la pneumothorax kwenye Upande wake wa Kushoto,

Pamoja na interstitial infiltrates kwenye mapafu yote mawili.

Hata hivo baada ya kufanyiwa kipimo cha computed tomography kilionyesha uwepo wa multiple cysts pamoja na Nodules kwenye eneo la Juu na kati kati ya Mapafu,

TIBA:

Mgonjwa huyu alitibiwa kwa kutumia chest-tube thoracostomy,

Kisha kuendelea na tiba ya dawa mbali mbali ikiwemo prednisone,

Na kushauriwa kuacha kabsa Uvutaji wa Sigara.

Baada ya Miezi Sita(6) ya follow-Up, Mgonjwa alikuwa ameacha kabsa Uvutaji wa Sigara, na alikuwa anaendelea kutumia low-dose ya prednisone, na Dalili zote zilipotea.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.