Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mazoezi ya kupunguza uzito na tumbo pamoja na Unene

Mazoezi ya kupunguza uzito na tumbo pamoja na Unene

Haya hapa ni Mazoezi ambayo unaweza kufanya ili Kupunguza Uzito,

Mazoezi haya unaweza kufanya ili kukusaidia kupunguza Uzito wako wa Mwili;

1. Kutembea, fahamu Kufanya mazoezi ya kutembea kwa zaidi ya nusu Saa kila siku huweza kusaidia kupunguza Uzito wa mwili,

kwani huweza kusaidia kuchoma zaidi ya Calories 150 mwilini,

Kadri unavyotembea kwa haraka na kwa muda mrefu zaidi ndivyo mwili wako huchoma Calories kwa haraka zaidi.

2. Kuruka kamba, Moja ya Mazoezi ambayo huweza kusaidia kupunguza Uzito kwa haraka sana ni pamoja na Zoezi la Kuruka kamba,

Njia hii ni rahisi na yaharaka kuchoma calories mwilini.

3. Fanya High Intensity Interval Training(HIIT) kama kwenye picha hapa chini

4. Fanya Zoezi ya Kuendesha Baiskeli,

Fahamu zoezi la Kuendesha Baiskeli huweza kusaidia Mwili kuchoma takribani Calories 400 mpaka 700 Mwilini,

Na hii ni pale ambapo unaendesha baiskeli kuanzia muda wa Saa Moja kutegemeana na Uzito wako wa Mwili, Kasi ya uendeshaji pamoja na aina ya uendeshaji.

5. Kuogelea, Pia kuogelea ni mojawapo ya zoezi ambalo husaidia sana kwenye kuboresha mzunguko wa damu kwenye Moyo na Mapafu,

Kupunguza hatari ya magonjwa kama vile; magonjwa ya Moyo, Kiharusi/Stroke, kisukari hasa type 2 diabetes, baadhi ya Saratani n.k,

Na pia husaidia kupunguza lehemu mbaya mwilini(Bad cholestrol) pamoja na shinikizo la damu(Blood pressure).

6. Fanya Zoezi la Streghth Training, hili ni zoezi kwa ajili ya kuimarisha misuli pamoja na nguvu mwilini,

ambapo kadri nguvu na Misuli huimarika ndivo uzito wa mwili hupungua.(Tazama kwenye picha)

7. Fanya Zoezi la Pilates(Tazama kwenye picha)

mfumo wa mazoezi kwa kutumia vifaa maalum ili kuboresha nguvu za mwili, kubadilika na mkao, na kuongeza ufahamu wa akili.

8. Fanya zoezi la kukimbia au Jogging,

Pia zoezi la Kukimbia maarufu kama Jogging ni mojawapo ya mazoezi mazuri sana kwa mtu ambaye anataka kupunguza Uzito.

9. Fanya Zoezi la Joga,

Hili ni zoezi ambalo huhusisha kiroho na kujinyima moyo, ambayo sehemu yake ni pamoja na udhibiti wa pumzi, kutafakari kwa kurelax, na kuhusisha mikao maalum ya mwili,

Hii hufanyika sana kwa ajili ya afya na utulivu.

10. Fanya Zoezi la Hiking, Hili ni zoezi maalum ambalo huhusisha Kutembea kwa miguu matembezi marefu,

hasa maeneo kama ya Porini n.k

11. Fanya Zoezi la Kupanda Ngazi,

Moja ya mazoezi mazuri kwa ajili ya kupunguza Uzito wako wa Mwili ni pamoja na kufanya zoezi la Kupanda ngazi.

[sc_fs_multi_faq headline-0=”h3″ question-0=”Aina ya Mazoezi ya Kufanya kila Siku” answer-0=”Fanya mazoezi haya kila siku,ruka kamba,kimbia,mazoezi ya kutembea,fanya angalau kwa nusu saa au Dakika 30 Kila Siku.” image-0=”” headline-1=”h3″ question-1=”Zipi ni faida za Kufanya Mazoezi?” answer-1=”Mazoezi husaidia sana kuimarisha mfumo wa kinga mwili na kutufanya tusipatwe na magonjwa kwa urahisi,mazoezi husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini,kutukinga na magonjwa kama vile kisukari,presha,magonjwa ya Moyo,Kusaidia kuondoa stress n.k” image-1=”” count=”2″ html=”true” css_class=””]

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.