athari za uti sugu kwa Mwanamke na Mwanaume
athari za uti sugu kwa Mwanamke na Mwanaume
Je, ni matatizo gani unaweza kuyapata baada ya kuwa na maambukizi ya muda mrefu kwenye njia ya mkojo?
Watu wanaougua UTI sugu wanaweza kupata matatizo mbali mbali,
Maambukizi ya mara kwa mara ya mfumo wa mkojo yanaweza kusababisha:
1. Maambukizi ya Figo,Matatizo ya figo au magonjwa ya figo,
ikiwemo na uharibifu wa kudumu wa figo, hasa kwa watoto wadogo
2. Maambukizi ya bacteria kwenye damu(sepsis),
ambayo huweza kupelekea hata mtu kupoteza maisha kutokana na maambukizi haya
Sepsis: hapa tunazungumzia hali mbaya inayotokana na kuwepo kwa microorganisms hatari katika damu au tishu nyingine na mwili kuanza kupambana kwa uwepo wao,
ambayo hali hii inaweza kusababisha utendaji mbaya wa viungo mbalimbali, mshtuko, na hata kifo.
3. septicemia, hali ambayo huhusisha bakteria tayari wameshaingia kwenye damu
4. kuongezeka kwa hatari ya kuzaa kabla ya wakati au kupata watoto wenye uzito wa chini au mdogo sana
5. Kuathiri mfumo wa uzazi kwa mwanaume na mwanamke n.k
Rejea Pia:
• Dalili za Uti Sugu kwa Mwanamke na Mwanaume, Soma hapa
• Other Source Link