Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Unaweza kupunguza hatari ya kupata Saratani kwa kufanya maamuzi sahihi

Unaweza kupunguza hatari ya kupata Saratani kwa kufanya maamuzi sahihi

Saratani ni nini?

Saratani,ni ukuaji wa seli usiowakawaida(abnormal cells growth),

ambapo baadhi ya seli huweza kuzaliana na kukua kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko kawaida kwenye maeneo mbali mbali mwilini.

Kwa Mujibu wa Shirika la afya Duniani(WHO):

Saratani ndyo chanzo kikuu cha VIFO duniani kote, ambapo karibu Vifo Million 10 ndani ya Mwaka 2020 pekee,vilitokana na Ugonjwa wa Saratani.

Ambapo aina hizi za Saratani,zikitajwa Kusababisha VIFO zaidi ndani ya Mwaka 2020;

  1. Saratani ya Mapafu-lung cancer (Vifo Million 1.80)
  2. Saratani ya Utumbo mpana-colon cancer pamoja na rectum cancer (Vifo 916 000)
  3. Saratani ya Ini-liver cancer (Vifo 830 000)
  4. Saratani ya Tumbo-stomach cancer (Vifo 769 000)
  5. Pamoja na Saratani ya Matiti-breast cancer (Vifo 685 000).

Hata hivo aina hizi hapa Chini za Saratani ziliongoza kuwapata Watu wengi zaidi ndani ya Mwaka 2020;

  1. Saratani ya Matiti-breast cancer(2.26 million cases);
  2. Saratani ya Mapafu-lung cancer(2.21 million cases);
  3. Saratani ya Utumbo mpana yaani colon cancer pamoja na rectum cancer (1.93 million cases);
  4. Saratani ya Tezi Dume-prostate cancer (1.41 million cases);
  5. Saratani ya ngozi-skin cancer (non-melanoma) (1.20 million cases); and
  6. Na Saratani ya tumbo-stomach cancer (1.09 million cases).

Watoto:Kuna takribani Vifo 28,000 na Cases Mpya 52,000 Za Saratani kwa Watoto, kwa Afrika ndani ya Mwaka 2020,

Huku takribani Watoto 400 000 wakipata Saratani Kila Mwaka.

Unaweza kubadilisha mtindo wa maisha,na kupunguza kwa kiwango kikubwa sana hatari ya wewe kupata Saratani mbali mbali,

Unaweza kupunguza hatari ya kupata Saratani kwa kufanya maamuzi sahihi kama vile;

1. Kuacha kabsa Uvutaji wa Sigara na matumizi ya Tumbaku(tobacco)

Saratani ya mapafu ni miongoni mwa Saratani zinazoongoza kusababisha vifo vingi Duniani,

Na uvutaji wa sigara ndio sababu kubwa ya Kuongeza hatari ya mtu kupata saratani hii ya mapafu(Lung cancer).

Matumizi ya tumbaku yanaweza kusababisha saratani karibu kwenye eneo lolote katika mwili wako.

Pia kwa Mtu ambaye anavuta moshi wa Sigara wakati wengine wakivuta Sigara yaani Secondhand Smokers huweza kupata Saratani ya mapafu pia,

kwani kuvuta ndani ule moshi wa Sigara ni kama na yeye ni mvutaji wa Sigara.

2. Kulinda Ngozi Yako,

Pia Saratani ya ngozi inaweza kusababishwa na Sababu za kimazingira zaidi,

Mionzi ya ultraviolet (UV) kutoka kwa jua inaonekana kuwa sababu muhimu zaidi ya kimazingira inayohusika na mtu kupata saratani ya ngozi,

Hivo basi,unashauriwa kuepuka kukaa kwenye Jua kali kwa Muda mrefu zaidi, jikinge na Jua kwa kuvaa nguo zinazokinga jua, kofia na miwani.

3. Kupunguza Unywaji wa Pombe,

Baadhi ya Tafiti zinaonyesha Kunywa pombe huongeza hatari ya kupata aina sita za saratani,

Kadiri unavyokunywa pombe kidogo, ndivyo hatari ya kupata saratani inavyopungua.

4. Dhibiti Uzito wako wa Mwili,

Uzito mkubwa au unene(Overweight/obesity) unahusishwa na hatari kubwa ya kupata aina 13 za saratani.

5. Kupima Hepatitis C,Hepatitis B n.k

Hepatitis ni tatizo linalohusisha kuvimba kwa ini, na kwa jina lingine hujulikana zaidi kama homa ya Ini.

Fanya vipimo hivi mara kwa mara kwani Hepatitis C ya muda mrefu inaweza kusababisha matatizo makubwa ya ini ikiwa ni pamoja na uharibifu wa ini, cirrhosis, kushindwa kwa ini, au saratani ya ini. N.K

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.