Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Dalili za kufeli kwa figo,Zipo dalili mbali mbali za kufeli kwa Figo

Dalili za kufeli kwa figo,Zipo dalili mbali mbali za kufeli kwa Figo

Kufeli kwa Figo

Kuna aina mbili za Kufeli kwa Figo ambazo ni;

  • acute kidney failure(tatizo la muda mfupi)
  • Pamoja na Chronic kidney failure(ugonjwa wa kudumu)

Sababu za Kufeli kwa Figo

Zipo Sababu mbali mbali ambazo huchangia tatizo la Kufeli kwa Figo ikiwemo;

– Matumizi ya Pombe Kupita kiasi

– Tatizo la Uzito mkubwa au unene

– Matumizi ya baadhi ya Dawa

– Magonjwa mbali mbali ikiwemo presha,sukari n.k

– Kuwa na tatizo lingine la uvimbe kwenye figo au kwa kitaalam huitwa Glomerulonephritis

– Kuwa na Ugonjwa ambao hujulikana kama Polycycystic Kidney Disease

Huu ni ugonjwa ambao huhusisha kuwepo kwa uvimbe kwenye figo zote mbili na mara nyingi ugonjwa huu unaweza kurithiwa kutoka kwa wazazi.

– Sababu zingine ambazo huchangia tatizo la kufeli kwa figo ni kama vile;

  • Umri mkubwa wa figo au Figo kuzeeka
  • Tatizo la kufunga kwa mishipa iendayo kwenye figo yaani kwa kitaalam hujulikana kama renal artery stenosis
  • Uwepo wa mawe kwenye Figo(Kidney Stones) ambayo huzuia Mkojo kupita
  • au uwepo wa tatizo la tezi dume iliyo karibu na kibofu
  • Tatizo la figo kuathiriwa na matumizi ya baadhi ya dawa
  • Tatizo la figo kushambuliwa na magonjwa ya mara kwa mara
  •  kwa watoto kupatwa na tatizo la kupungua ukubwa wa figo na mwisho mkojo kurudi nyuma n.k.

Katika Makala hii tunajadili Zaidi kuhusu Dalili za kufeli kwa figo,Soma Zaidi hapa..!!!

Dalili za kufeli kwa figo

Kwa Mujibu wa Vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa-Centers for Disease Control and Prevention (CDC),

Tatizo la kufeli kwa Figo linaweza lisionyeshe dalili zozote endapo ni hatua za awali kabsa,

Huku asilimia 90% ya watu wenye tatizo la kufeli kwa figo ambalo ni lakudumu(chronic kidney failure) hawajui kama wana tatizo hili.

Lakini kadri Ugonjwa unavyoendelea,ndivyo dalili huanza Kujitokeza, na Dalili hizo za kufeli kwa figo ni pamoja na;

– Kupungua kwa kiwango cha Mkojo

– Kuvimba Miguu, Hii pia ni mojawapo ya Dalili za kufeli kwa figo,

Hii hutokana na kuongezeka kwa kiwango cha maji mwilini hasa kutokana na Figo kufeli au kushindwa kutoa maji kama taka mwili nje kwa njia ya Mkojo.

– Kupata shida ya kukosa Pumzi

– Mwili kukosa nguvu pamoja na Kuchoka kupita kiasi

– Kuhisi hali ya kichefuchefu ambacho hakiiishi

– Wakati mwngine kupata maumivu kifuani

Kupoteza fahamu(Coma) n.k

Dalili za kufeli kwa figo

Dalili za kufeli kwa figo kwa Muda mfupi(acute kidney failure) ni Pamoja na;

– Kupungua kiwango cha Mkojo unaokojoa,

Ingawa kuna wakati hali hii hupotea

– Maji kujikusana zaidi mwilini na Kusababisha Kuvimba kwa miguu n.k

– Kukosa pumzi(Shortness of breath)

– Mwili kukosa nguvu na kuchoka Sana

– Kuhisi hali ya kichefuchefu mara kwa mara

– Mapigo ya moyo kubadilika

– Kupata maumivu ya kifua,

– Na wakati mwngine kupoteza fahamu

Madhara ya kufeli kwa Figo

Kufeli kwa figo, kunaweza kuleta shida mbali mbali mwilini kama vile;

• kuongezeka kwa maji mwilini na kusababisha uvimbe mfano; Uvimbe wa Miguu n.k

• viwango vya asidi kuongezeka,

• viwango vya potasiamu kuongezeka

• viwango vya kalsiamu kuongezeka

• viwango vya phosphate kuongezeka

• Na katika hatua za baadaye, upungufu wa damu mwilini hutokea

• Pamoja na Kifo

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je, kuna aina ngapi za kufeli kwa Figo?

Kuna aina mbili za Kufeli kwa Figo ambazo ni;

  • acute kidney failure(tatizo la muda mfupi)
  • Pamoja na Chronic kidney failure(ugonjwa wa kudumu)

Hitimisho

Dalili za kufeli kwa figo ni Pamoja na;

Kupungua kiwango cha Mkojo unaokojoa,Ingawa kuna wakati hali hii hupotea

-Maji kujikusana zaidi mwilini na Kusababisha Kuvimba kwa miguu n.k

– Kukosa pumzi(Shortness of breath)

– Mwili kukosa nguvu na kuchoka Sana

– Kuhisi hali ya kichefuchefu mara kwa mara

– Mapigo ya moyo kubadilika

– Kupata maumivu ya kifua,

– Na wakati mwngine kupoteza fahamu n.k

Ukiona dalili kama hizi hakikisha unawahi hospital kwa ajili ya VIPIMO Zaidi.

NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.