Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Dalili za saratani ya matiti kwa wanawake

Dalili za saratani ya matiti kwa wanawake

SARATANI NI NINI?

Saratani ni hali ya ukuaji wa seli hai za mwili usio wakawaida au ulizidi kiwango,Kwahyo basi, Saratani ya matiti ni ugonjwa unaohusisha ukuaji usio wa kawaida wa seli hai zilizopo au zinazounda eneo la titi au matiti.

Katika Makala hii tunajadili zaidi kuhusu dalili za saratani ya matiti kwa wanawake,Ingawa unatakiwa kufahamu kwamba, hata Wanaume pia hupata Saratani ya matiti.

Dalili za saratani ya matiti kwa wanawake

Zipo baadhi ya Dalili za saratani ya matiti kwa wanawake ambazo ni muhimu sana kuzifahamu mapema, soma zaidi hapa kufahamu

(1) Dalili ya awali inayoweza kutambulisha saratani ya matiti kwa Wanawake ni kuwepo kwa uvimbe kwenye titi ambao huwa na hali tofauti na sehemu nyingine za titi.

Hata hivyo, si kila uvimbe kwenye titi unaashiria uwepo wa saratani ya matiti kwa wanawake,

Uvimbe huu huwa mgumu, unaochezacheza kwenye titi, ambapo wakati mwingine unaweza kuwa na maumivu makali au kusiwe na maumivu yeyote.

Wakati mwingine Wataalam wa afya huweza kufananisha uwepo wa kitu kama punje ya harage au mchele kwenye titi lako,

Uvimbe huu huwepo zaidi ya mzunguko mmoja wa hedhi kwa wale ambao hawajaacha kupata hedhi.

• Dalili zingine za Saratani ya matiti kwa Wanawake ni pamoja na;

(2) Kuwepo kwa uvimbe kwenye sehemu za kwapa

(3) Sehemu ya titi kuingia ndani inayoashiria uvimbe usioonekana au usioweza kuhisiwa

(4) Mabadiliko kwenye chuchu, kama vile;

  • chuchu kuzama ndani au kuwa na nundu ndogo ndogo,
  • chuchu kuwasha,
  • kuhisi kama kuchoma,
  • kidonda kwenye chuchu
  • au chuchu kuwa na kovu ambalo huashiria saratani ya sehemu hiyo

(5)Dalili nyingine za saratani ya matiti kwa wanawake ni pamoja na

Kubadilika kwa umbo la titi, ngozi ya titi kuwa kama ganda la chungwa (peu de orange), ngozi kuwa na rangi nyekundu, na kuongezeka kwa joto kwenye titi. Dalili hizi huashiria kusambaa kwa saratani mwilini.

(6) Dalili nyingine ni chuchu kutoa maji yasiyo ya kawaida ambayo hayana rangi. Aidha wakati mwingine, chuchu hutokwa damu au majimaji yenye rangi nyingine tofauti. n.k

Hizo ndyo baadhi ya Dalili za saratani ya matiti kwa wanawake.

MAMBO YANAYOONGEZA HATARI YA KUPATA SARATANI YA MATITI KWA WANAWAKE

(1) Kuanza hedhi katika umri mdogo.

(2) Kukoma siku Za hedhi katika umri mkubwa

(3) Kutozaa kabisa.

(4) Kutonyonyesha kabisa au kunyonyesha kwa muda mfupi.

(5) Utumiaji mafuta mengi katika chakula.

(6) Kutokufanya mazoezi ya mara kwa mara.

(7) Uzito mkubwa au Unene kupita kiasi(Overweight/obesity)

(9) Uvutaji wa sigara.

(10) Utumiaji wa pombe kupita kiasi.

(11) Historia ya saratani ya matiti katika familia. n.k

JINSI YAKUJILINDA NA SARATANI YA MATITI KWA WANAWAKE

✓ Kujichunguza mwenyewe mara kwa mara kwa mara.

✓ Uchunguzi wa kitabibu wa matiti kila mwaka.

✓ Uchunguzi wa matiti kwa njia ya mashine ya mionzi (mara moja kwa mwaka kwa wenye miaka zaidi ya 40).

✓ Wanawake wote wenye umri kuanzia miaka 21 wajichunguze matiti yao siku ya 5-7 baada ya kumaliza hedhi mbele ya kioo

Madhara ya saratani ya Matiti kwa Wanawake

Madhara ya saratani ya matiti kwa wanawake ni Pamoja na;

  • Titi kuoza na kukatwa kabsa
  •  Titi kuuma sana na kutoa damu au usaha kila wakati
  • Kushindwa kabsa kunyonyesha kama mama ananyonyesha
  •  Mwanamke kupoteza maisha pia

Hitimisho

Ni muhimu sana kufahamu kuhusu Dalili za saratani ya matiti kwa wanawake,ili endapo utaona Viashiria vyovyote vya Saratani hii ya matiti upate matibabu Mapema,

Dalili za saratani ya matiti kwa wanawake ni pamoja na;

(1) kuwepo kwa uvimbe kwenye titi ambao huwa na hali tofauti na sehemu nyingine za titi.

Hata hivyo, si kila uvimbe kwenye titi unaashiria uwepo wa saratani ya matiti kwa wanawake,

Uvimbe huu huwa mgumu, unaochezacheza kwenye titi, ambapo wakati mwingine unaweza kuwa na maumivu makali au kusiwe na maumivu yeyote.

Wakati mwingine Wataalam wa afya huweza kufananisha uwepo wa kitu kama punje ya harage au mchele kwenye titi lako,

Uvimbe huu huwepo zaidi ya mzunguko mmoja wa hedhi kwa wale ambao hawajaacha kupata hedhi.

• Dalili zingine za Saratani ya matiti kwa Wanawake ni pamoja na;

(2) Kuwepo kwa uvimbe kwenye sehemu za kwapa

(3) Sehemu ya titi kuingia ndani inayoashiria uvimbe usioonekana au usioweza kuhisiwa

(4) Mabadiliko kwenye chuchu, kama vile;

  • chuchu kuzama ndani au kuwa na nundu ndogo ndogo,
  • chuchu kuwasha,
  • kuhisi kama kuchoma,
  • kidonda kwenye chuchu
  • au chuchu kuwa na kovu ambalo huashiria saratani ya sehemu hiyo

(5)Dalili nyingine za saratani ya matiti kwa wanawake ni pamoja na

Kubadilika kwa umbo la titi, ngozi ya titi kuwa kama ganda la chungwa (peu de orange), ngozi kuwa na rangi nyekundu, na kuongezeka kwa joto kwenye titi. Dalili hizi huashiria kusambaa kwa saratani mwilini.

(6) Dalili nyingine ni chuchu kutoa maji yasiyo ya kawaida ambayo hayana rangi. Aidha wakati mwingine, chuchu hutokwa damu au majimaji yenye rangi nyingine tofauti. n.k

Hizo ndyo baadhi ya Dalili za saratani ya matiti kwa wanawake, Ukiona dalili kama hizi wahi Mapema Hospitalini kwa ajili ya UCHUNGUZI na Matibabu Zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.