Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Dalili magonjwa ya zinaa,Soma hapa kufahamu

Dalili magonjwa ya zinaa,Soma hapa kufahamu

Magonjwa ya Zinaa

Magonjwa ya Zinaa ni yale magonjwa yote ambayo unaweza kuyapata kwa kufanya mapenzi au wakati wa kufanya mapenzi(sexual contact).

Vimelea vya magonjwa kama vile bacteria, viruses au parasites ambavyo husababisha magonjwa ya Zinaa huweza kupita kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia vitu kama vile;

  • Damu
  • Manii au semen,
  • Maji maji ukeni(vaginal fluids)
  • Au maji maji kutoka sehemu zingine za mwili

Wakati mwingine maambukizi ya magonjwa ya zinaa huweza kusambazwa kwa njia ambazo sio za kujamiiana,

Mfano; kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito au wakati wa kujifungua,

Wakati wa uchangiaji damu au kwa kushirikiana vifaa vya ncha kali kama vile sindano n.k

Yapo magonjwa mbali mbali ya Zinaa ikiwemo;

  • Ugonjwa wa Kisonono
  • Ugonjwa wa kaswende
  • Ugonjwa wa chlamydia
  • Maambukizi ya human papilloma virus(HPV)
  • Trichomoniasis n.k

Katika Makala hii tumechambua baadhi ya Dalili za magonjwa ya zinaa,Soma hapa.

Dalili magonjwa ya zinaa

Magonjwa ya zinaa sio kila wakati huonyesha dalili, Inawezekana kuambukizwa magonjwa ya zinaa kutoka kwa watu wanaoonekana kuwa na afya njema kabisa na hata wasijue kuwa wana maambukizi.

Dalili za magonjwa ya zinaa

Kwa Ujumla hizi hapa ni baadhi ya dalili za magonjwa ya Zinaa bila kuangalia ugonjwa mmoja mmoja;

– Kuwa na Vidonda kwenye sehemu za siri au katika eneo la mdomo au haja kubwa

– Kuwa na upele au madoa madoa kwenye ngozi,

hii pia huweza kuwa mojawapo ya dalili za magonjwa ya zinaa kama vile ugonjwa wa kaswende n.k

– Kupata maumivu wakati wa Kukojoa au kuhisi kuungua wakati wa kukojoa

– Kutokwa na uchafu kwenye uume, uchafu kama usaha,

Hii pia ni mojawapo ya dalili za magonjwa ya Zinaa kama vile ugonjwa wa kisonono n.k

– Kutokwa na uchafu usio wa kawaida au wenye harufu mbaya ukeni

– Kutokwa na damu kwa uke kusiko kawaida

– Kupata Maumivu wakati wa tendo la ndoa

– Kuwa na Vidonda, lymph nodes kuvimba, haswa kwenye kinena lakini wakati mwingine zinaenea zaidi

– Kupata Maumivu ya chini ya tumbo

– Kupata Homa

– kuwa na Upele kwenye ngozi, mikononi au miguuni n.k

Hizi ni baadhi tu ya dalili za magonjwa ya Zinaa,

Ishara na dalili za magonjwa ya zinaa zinaweza kuonekana siku chache baada ya mtu kupata magonjwa ya Zinaa.

Hata hivyo, wakati mwingine inaweza kuchukua miaka kabla ya kuwa na matatizo yoyote yanayoonekana(pasipo kuonyesha dalili), kulingana na aina ya vimelea vinavyosababisha magonjwa ya zinaa.

Hitimisho

Magonjwa ya Zinaa ni yale magonjwa yote ambayo unaweza kuyapata kwa kufanya mapenzi au wakati wa kufanya mapenzi(sexual contact),

Wakati mwingine maambukizi ya magonjwa ya zinaa huweza kusambazwa kwa njia ambazo sio za kujamiiana,Mfano; kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito au wakati wa kujifungua,

Yapo magonjwa mbali mbali ya Zinaa ikiwemo;

  • Ugonjwa wa Kisonono
  • Ugonjwa wa kaswende
  • Ugonjwa wa chlamydia
  • Maambukizi ya human papilloma virus(HPV)
  • Trichomoniasis n.k

Kwa Ujumla hizi hapa ni baadhi ya dalili za magonjwa ya Zinaa bila kuangalia ugonjwa mmoja mmoja;

– Kuwa na Vidonda kwenye sehemu za siri au katika eneo la mdomo au haja kubwa

– Kuwa na upele au madoa madoa kwenye ngozi,

hii pia huweza kuwa mojawapo ya dalili za magonjwa ya zinaa kama vile ugonjwa wa kaswende n.k

– Kupata maumivu wakati wa Kukojoa au kuhisi kuungua wakati wa kukojoa

– Kutokwa na uchafu kwenye uume, uchafu kama usaha,

Hii pia ni mojawapo ya dalili za magonjwa ya Zinaa kama vile ugonjwa wa kisonono n.k

– Kutokwa na uchafu usio wa kawaida au wenye harufu mbaya ukeni

Ukiona dalili hizi hakikisha unapata msaada wa Matibabu

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.