Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Magonjwa hatari kwa mama mjamzito

Magonjwa hatari kwa mama mjamzito

Maambukizi hatari sana yanaweza yasitokee mara kwa mara wakati wa ujauzito,bakteria na virusi vingi haviwezi kumdhuru mtoto wako,

Hata hivyo,Sio wakati wote ni hivo,Yapo Magonjwa hatari kwa mama mjamzito,ambayo huweza kusababisha madhara makubwa sana kwa mama mjamzito pamoja na mtoto tumboni.

Magonjwa hatari kwa mama mjamzito

Mambo mahususi yanayoweza kuchangia mimba kuwa katika hatari kubwa ni pamoja na:

1. Kubeba mimba kwenye umri mkubwa zaidi, mfano zaidi ya miaka 35.

2. Mtindo mbaya wa maisha, kama vile;

  • uvutaji wa Sigara kipindi cha ujauzito
  • Unywaji wa pombe kipindi cha ujauzito
  • Au kutumia dawa zozote za kulevyia

2. Mama mjamzito kuwa na matatizo ya kiafya kama vile;

  • Shinikizo la damu kali,
  • unene kupita kiasi,
  • kisukari,
  • kifafa,
  • magonjwa ya tezi,
  • matatizo ya moyo au damu,
  • pumu isiyodhibitiwa vizuri,
  • na maambukizi yanayoweza kuongeza hatari ya ujauzito,Mishipa ya damu na mtoto.

3. matatizo yanayojitokeza wakati wa ujauzito yanaweza kuwa hatari. Mifano ni pamoja na tatizo kwenye kondo la nyuma au placenta isiyo ya kawaida,

4. ukuaji duni wa mtoto chini ya asilimia 10 kwa umri wa ujauzito (upungufu wa ukuaji wa mtoto)

5. na utambuzi wa Rh sensitization – hali hatari ambayo inaweza kutokea wakati kundi lako la damu ni Rh factor NEGATIVE AU hasi na kundi la damu la mtoto wako ni Rh factor POSITIVE au chanya.

6. Ujauzito wa watoto zaidi ya mmoja. Hatari ya ujauzito ni kubwa kwa wanawake wanaobeba zaidi ya mtoto nmoja.

Ujauzito wa mapacha pia una hatari kubwa zaidi kuliko ujauzito wa mtoto mmoja.

7. Historia ya ujauzito. Historia ya matatizo ya shinikizo la damu yanayohusiana na ujauzito, kama preeclampsia, huongeza hatari ya kuwa na ugonjwa huu wakati wa ujauzito ujao.

Historia ya ujauzito pia inaweza kuongeza hatari ya matatizo wakati wa ujauzito ujao. Kama umewahi kupata shinikizo la damu wakati wa ujauzito au kujifungua kabla ya wakati, unaweza kuwa na hatari ya kupata matatizo hayo tena wakati wa ujauzito ujao,

Ikiwa ulijifungua kabla ya wakati wako katika ujauzito wako uliopita una hatari ya kujifungua mapema katika ujauzito wako ujao. Ongea na mtoa huduma za afya kuhusu historia yako kamili ya uzazi.

Magonjwa yanayoweza kudhuru Mtoto wakati wa ujauzito au kujifungua

Hapa chini unaweza kusoma kuhusu magonjwa fulani yanayoweza kudhuru mtoto wakati wa ujauzito au kujifungua.

1. Rubella

Rubella ni maambukizi ya virusi, Ikiwa unapata maambukizi haya ya Rubella kwenye miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito, au haukuwahi kupata ugonjwa huu hapo awali na haukupata chanjo, Hii inaweza kumdhuru mtoto.

Mara nyingine inaweza kusababisha

  • kuharibika kwa mimba
  • au kuharibu ubongo, masikio, na moyo wa mtoto.

Wanawake ambao hawakupata chanjo ya kuzuia Rubella wanapaswa kupata chanjo kabla ya kupanga ujauzito.

2. Toxoplasmosis na listeria
Kuna maambukizi mawili yanayoweza kuenezwa kupitia chakula na ni hatari sana wakati wa ujauzito: listeria na toxoplasmosis.

Hatari ya kupata maambukizi haya ni ndogo sana, lakini ikiwa utapata maambukizi haya kwa hali mbaya zaidi inaweza kusababisha kuharibika kwa mimba.

Magonjwa kadhaa kama rubella, toxoplasmosis, herpes na group B streptococcus yanaweza kudhuru mtoto wakati wa ujauzito au kujifungua. Ni muhimu kuchukua tahadhari kwa kufuata miongozo ya lishe salama wakati wa ujauzito na kushauriana na daktari kuhusu jinsi ya kuzuia au kutibu magonjwa haya.

Kwa mfano, rubella ni ugonjwa hatari unaoweza kusababisha mtoto kuzaliwa na matatizo ya ubongo, masikio na moyo. Wanawake wasiowahi kupata ugonjwa huu au kuchanjwa wanashauriwa kupata chanjo kabla ya kupanga ujauzito.

Kwa hiyo, ni muhimu kuzingatia miongozo ya afya wakati wa ujauzito ili kuhakikisha afya bora ya mama na mtoto.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.