Siku ya Shinikizo la damu duniani,Shinikizo la damu na kushindwa kwa moyo
Siku ya Shinikizo la damu duniani,
Shinikizo la damu limetajwa kuwa chanzo cha magonjwa mengi yanayohusiana na kushindwa kwa moyo.
Shinikizo la damu limetajwa kuwa chanzo cha magonjwa mengi yanayohusiana na kushindwa kwa moyo kufanya kazi yake. Shirika la afya duniani, WHO linaeleza kuwa mtu mmoja kati ya watu wazima watatu ana shinikizo la damu,
na wengi wao hawajitambui kwa kuwa ni mara chache dalili kujitokeza.
Na zaidi ya yote nusu ya vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo au kiharusi hutokana na shinikizo la damu na mwelekeo ni kwamba hali itazidi kuwa mbaya iwapo hatua hazitachukuliwa.