Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA FIGO KUFELI AU KUSHINDWA KUFANYA KAZI(KIDNEY FAILURE),CHANZO,DALILI,NA MATIBABU

Ugonjwa wa kufeli kwa figo

Katika Makala hii tunachambua zaidi kuhusu ugonjwa wa kufeli kwa figo,chanzo,dalili,madhara pamoja na Matibabu yake.

Ugonjwa wa kufeli kwa figo ni ugonjwa ambao huwapata watu wengi na sababu kubwa zikitokana na mtindo mbaya wa maisha ikiwemo ulaji mbaya,matumizi ya pombe kupita kiasi,Uvutaji wa Sigara, tatizo la kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi,matumizi ya baadhi ya dawa,kutokufanya mazoezi n.k

Ugonjwa wa kufeli kwa figo unaweza kuleta shida mbali mbali mwilini kama vile;

  • kuongezeka kwa maji mwilini na kusababisha uvimbe mfano; Uvimbe wa Miguu n.k
  •  viwango vya asidi kuongezeka, 
  • viwango vya potasiamu kuongezeka
  • viwango vya kalsiamu kuongezeka
  • viwango vya phosphate kuongezeka
  •  Na katika hatua za baadaye, upungufu wa damu mwilini hutokea.

Aina za Ugonjwa wa kufeli kwa figo

 Kuna Aina mbili kuu za ugonjwa wa kufeli kwa figo  ambazo ni;

(i) Figo kushindwa kufanya kazi ndani ya mda mfupi kwa kitaalam tunaita Acute kidney Failure,

ambayo hutokana na Figo kuumia gafla na mara nyingi mgonjwa hupata matibabu ya kutosha na hali ikawa sawa

(ii) Figo kushindwa kufanya kazi au kuwa na ugonjwa sugu wa figo ambapo kitaalam hujulikana kama Chronic kidney failure ambao mara nyingi hauwezi kutibika kabsa.

  Katika aina  zote mbili,kuna sababu ya msingi zinazochangia Ugonjwa wa kufeli kwa figo;

Chanzo cha Ugonjwa wa kufeli kwa figo

Sababu kubwa  za kuwa na ugonjwa wa kufeli kwa figo ni pamoja na;

1. Ugonjwa wa Kisukari:

Ugonjwa wa Kisukari ni miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia kutokea kwa ugonjwa wa kufeli kwa figo,

Tafiti zinaonyesha Asilimia 35% mpaka 40% ya magonjwa ya figo yasiyopona yote husababishwa na ugonjwa kisukari.

Ambapo ni sawa na kusema katika kila watu watatu(3) walio na ugonjwa wa kisukari, mmoja(1) wao anaweza kupata ugonjwa sugu wa figo.

2. Tatizo la Presha au shinikizo la damu:

Ugonjwa wa Presha au Shinikizo la damu usipodhibitiwa vizuri,huweza kuwa chanzo kikubwa cha ugonjwa wa kufeli kwa figo au figo kushindwa kufanya kazi,

Tafiti zinasema Asilimia 30% ya magonjwa ya figo yasiyopona husababishwa na shinikizo la damu. 

3. Kuwa na tatizo lingine la uvimbe kwenye figo au kwa kitaalam huitwa Glomerulonephritis

Tatizo hili la Glomerulonephritis ni la tatu katika kusababisha magonjwa sugu ya figo likiwemo hili la Figo kufeli au kushindwa kufanya kazi.

4. Ugonjwa ambao hujulikana kama Polycycystic Kidney Disease 

Huu ni ugonjwa ambao huhusisha kuwepo kwa uvimbe kwenye figo zote mbili na mara nyingi ugonjwa huu unaweza kurithiwa kutoka kwa wazazi.

5. Sababu zingine za kutokea kwa Ugonjwa wa kufeli kwa figo ni pamoja na;

  • Umri mkubwa wa figo au Figo kuzeeka
  • Tatizo la kufunga kwa mishipa iendayo kwenye figo yaani kwa kitaalam hujulikana kama renal artery stenosis
  • Uwepo wa mawe ya Figo(Kidney Stones) ambayo huzuia Mkojo kupita au uwepo wa tatizo la tezi dume iliyo karibu na kibofu
  • Tatizo la figo kuathiriwa na matumizi ya baadhi ya dawa
  • Tatizo la figo kushambuliwa na magonjwa ya mara kwa mara
  •  kwa watoto kupatwa na tatizo la kupungua ukubwa wa figo na mwisho mkojo kurudi nyuma.

 Utambuzi wa ugonjwa wa kufeli kwa figo

Ugonjwa wa kufeli kwa figo husababishwa na kupungua kwa uwezo cha kuchuja ndani ya glomerular, ambapo tunazungumzia kiwango cha damu ambacho huchujwa kwenye glomeruli ya figo.  Hii hugunduliwa baada ya kupungua kwa au kutokuwepo kwa uzalishaji wa mkojo au taka mwili (creatinine au urea) katika damu.  Kulingana na sababu hizo,  Hali ya hematuria yaani kutoka  kwa damu kwenye mkojo na proteinuria (upotezaji wa protini kwenye mkojo) inaweza kutokea.

Dalili za Ugonjwa wa kufeli kwa figo

?DALILI ZA UGONJWA WA KUFELI KWA FIGO-KIDNEY FAILURE

 Dalili Za Ugonjwa wa kufeli kwa figo zinaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu, baadhi ya dalili hizo ni pamoja na;

(1) Tatizo la Kuvimba uso,Miguu na tumbo

Tatizo la Kuvimba uso, miguu na tumbo, ni ishara za ugonjwa wa kufeli kwa figo, Japo si kila uvimbe hutokana na tatizo la kufeli kwa Figo(kidney failure).

(2) Tatizo la Kukosa hamu ya chakula, kichefuchefu, na kutapika

Tatizo la Kukosa hamu ya chakula huweza kumpata mtu mwenye ugonjwa wa kufeli kwa figo,

hii hutokana na uwepo wa sumu nyingi hivo kuleta hali ya kichefuchefu, kutapika na kwikwi.

(3) Kupata tatizo la presha au Shinikizo la damu 

Tatizo hili ni kawaida sana kwa wagonjwa wa Figo kufeli.

(4)Tatizo la ukosefu wa damu

Kupatwa na hali ya udhaifu na kuchoka mapema, pamoja na dalili zingine za upungufu wa damu

(5) Tatizo la kupata maumivu ya mgongo,kujikuna na maumivu ya miguu (cramps) pamoja na  Maumivu wakati wa kukojoa

Dalili zingine zinazohusu mkojo ni pamoja na:

1. Kiwango cha Mkojo kupungua

2. Kupata Muwasho wakati wa kukojoa 

3. kukojoa mara kwa mara

4. kukojoa damu au usaha

5. Ugumu wa kukojoa

Cr: To Kidney education

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.