Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

WHO imetangaza washindi wa Tamasha la 4 la Filamu ya Afya kwa Wote(4th Health for All Film Festival)

WHO imetangaza washindi wa Tamasha la 4 la Filamu ya Afya kwa Wote(4th Health for All Film Festival)

Saba(7) kushinda filamu fupi, Wanne(4) kutajwa kwenye category maalum kutoka  kwenye baraza la waamuzi

Shirika la Afya Duniani(WHO) limetangaza uteuzi rasmi wa filamu zilizoshinda mwaka huu katika Tamasha lake la 4 la Mwaka la Afya kwa Wote(4th Health for All Film Festival), lililofanyika Makao Makuu ya WHO, Geneva.

Hafla hiyo, iliyohudhuriwa na waigizaji, watayarishaji na watu mashuhuri, wakishuhudia filamu zilizoshinda zikitangazwa kwa kategori 7 tofauti, huku filamu 4 zikitajwa maalum kabsa kutoka kwa baraza la waamuzi.

Huu ni mwaka wa nne wa tamasha la filamu na ushindani ulikuwa mkali zaidi, na baadhi ya filamu 93 zilizoorodheshwa zikiangazia masuala kuanzia wasiwasi na mfadhaiko hadi athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa afya, pamoja na changamoto za kiafya za watu wenye ulemavu.

Filamu hizo zilifanyiwa tathimini na jopo la wataalamu mashuhuri, wasanii na wanaharakati, wakiwemo waigizaji mashuhuri, Sharon Stone na Alfonso Herrera, mwandishi wa densi, Sherrie Silver, mwanaharakati wa hali ya hewa, Sophia Kianni na mwanahabari, Adelle Onyango,

Pia Walijumuishwa na maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa WHO.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema. “Kusikiliza sauti za watu walioathiriwa na masuala ya afya ni njia nzuri ya kuongeza ufahamu na kuboresha uelewa wetu na hii inaweza kutusaidia kusonga mbele kuelekea afya kwa wote.”

Anaeleza zaidi hapa chini;

“The Health for All Film Festival brings a human face to WHO’s scientific work,” said WHO Director-General, Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus. “Listening to the voices of people affected by health issues is a powerful way to raise awareness and improve our understanding of people’s experiences and this can help us advance towards health for all.”

Sharon Stone, Golden Globe na mwigizaji aliyeshinda tuzo ya Emmy kutoka Marekani, mtayarishaji na mwanaharakati wa masuala ya afya na kibinadamu alisema:

“I am delighted to be part of the Health for All Film Festival. This is about creating better awareness on crucial actions needed for reaching healthier living conditions around the world. The stories selected talk to us about the intrinsic value of good health and its access, and they advocate for universal health coverage. Universal Health Coverage is a very important right, it’s a human right for everyone around the world.”

Zawadi nne maalum pia zilitolewa kwa ajili ya filamu iliyotayarishwa na Wanafunzi, filamu ya Mabadiliko ya Tabia ya nchi na Afya, filamu ya Afya na Haki za Kijinsia na Uzazi pamoja na Filamu Fupi Sana.

Filamu nyingine iliyoshinda, ni kutoka Bangladesh, Filamu hii ina mvulana mdogo kwenye mazingira hatarishi ya Lead kutoka kwenye kiwanda(local factory),Filamu hiyo ya kusisimua inaeleza juu ya madhara kwa maendeleo yake ya elimu na kazi ambayo shirika lisilo la kiserikali la eneo hilo limefanya,

Shirika hilo limefanya vitu viwili, kwanza kuangazia suala hilo na kisha kuchukua hatua ya kuzuia sumu ya risasi(lead poisoning) katika jamii iliyoathiriwa.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.