Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Silvio Berlusconi, waziri mkuu wa zamani wa Italia amefariki dunia

Silvio Berlusconi, waziri mkuu wa zamani wa Italia amefariki dunia.

Silvio Berlusconi wa Italia afariki baada ya kuugua mara kadhaa,
Mfanyabiashara huyo bilionea alibadilisha hali ya kisiasa ya Italia, mara nyingi huku akizuia kashfa za kisheria na Skendo za ngono.

Mfanyabiashara huyo bilionea aliunda kampuni kubwa zaidi ya vyombo vya habari nchini Italia kabla ya kubadilisha hali ya kisiasa – huku akikabiliana na kashfa nyingi za kisheria na ngono.

Madaktari walisema Berlusconi wa Italia alikuwa na tatizo la saratani ya damu(leukaemia), na Alikuwa akiumwa mara kadhaa katika miezi ya hivi karibuni,

Alilazwa hospitalini mnamo mwaka 2020 baada ya kuambukizwa COVID-19, akielezea tatizo hili kama “shida ngumu zaidi katika maisha yake”.

Mnamo Aprili 2023, madaktari walifichua kuwa alikuwa katika uangalizi mkubwa akiugua saratani ya damu na maambukizi ya mapafu.

Alilazwa katika hospitali ya Milan siku ya Ijumaa kwa kile wasaidizi walisema ni vipimo vilivyopangwa vilivyohusiana na saratani yake ya damu(leukaemia).

Kifo cha Berlusconi kinaacha “Pengo kubwa” kwa sababu alikuwa mtu mashuhuri, waziri wa ulinzi wa Italia Guido Crosetto alisema kwenye Twitter siku ya Jumatatu.

“I loved him very much. Farewell Silvio,” Crosetto wrote.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.