Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
MagonjwaUtafiti

Dawa ya Kisukari Metformin Inapunguza Hatari ya kupata COVID ya Muda mrefu, Utafiti Unasema

Dawa ya Kisukari Metformin Inapunguza Hatari ya kupata COVID ya Muda mrefu, Utafiti Unasema

Metformin, dawa ambayo hutumiwa kwenye matibabu ya kisukari aina ya 2(type 2 diabetes), hupunguza sana hatari ya mtu ya kupata COVID ya Muda mrefu baada ya kuambukizwa, kulingana na utafiti uliochapishwa kwenye jarida la “The Lancet“.

Washiriki wa utafiti ambao walitumia metformin walikuwa na uwezekano mdogo wa kupata COVID(long COVID) kwa zaidi ya asilimia 40% kuliko wale waliopokea placebo, watafiti waligundua.

Washiriki wa utafiti ambao walianza kutumia metformin chini ya siku nne baada ya dalili za COVID kuanza walipunguza hatari ya kupata COVID ya muda mrefu kwa asilimia 63%.

“Matokeo ya utafiti huu ni muhimu kwa sababu COVID ya muda mrefu inaweza kuwa na athari kubwa kwa maisha ya watu,” Carolyn Bramante, MD, mpelelezi mkuu na profesa msaidizi katika Shule ya Matibabu ya Chuo Kikuu cha Minnesota, alisema katika taarifa ya habari.

“Metformin ni dawa ya bei nafuu, salama na inayopatikana kwa urahisi, na matumizi yake kama hatua ya kuzuia yanaweza kuwa na matokeo makubwa kwa afya ya umma.”

Zaidi ya watu 1,200 waliochaguliwa bila mpangilio maalum katika tovuti sita za Marekani walishiriki katika utafiti huo,

Walipewa metformin au placebo, pamoja na sehemu ndogo ya washiriki wanaotumia ivermectin, fluvoxamine, au placebos zao.

Washiriki walikuwa kati ya umri wa miaka 30 na 85, Nusu yao walikuwa wamechanjwa na hakuna aliyekuwa ameambukizwa COVID.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.