Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA CORONA

  UGONJWA WA CORONA NA UJAUZITO

➡️ Ombeni Mkumbwa

Soma Makala hii ya Ugonjwa wa Corona au COVID19 na Ujauzito au Mimba,Lengo kuu likiwa kuelimishana na Kupeana Maarifa Zaidi.


⚠️ Je, COVID-19 ni nini?


COVID-19 ni maambukizi ambayo husababishwa na virusi vinavyoitwa Corona, virusi hivi ni kama virusi vinavyosababisha Ugonjwa wa mafua ya kawaida. Na kama yalivyo mafua,ugonjwa huu hutesa sana kwa mtu mwenye matatizo mengine kwenye Mfumo wake wa hewa.

BAADHI YA DALILI ZA COVID-19 AU CORONA

(1) Kuwa na homa kali

(2) kikohozi au kuhisi kuishiwa na pumzi. 

(3) Matatizo ya kupumua na kubanwa mbavu

(4) Mafua makali yanayoambatana na Kichwa kuuma sana

(5) Kupiga Chafya za mara kwa mara n.k


? NJIA ZA KUENEZA COVID-19 AU CORONA

– Kwa Njia ya hewa na Kuwa karibu na mtu mwenye virusi hivi na kushika vifaa vyovyote vilivyoshikwa na mtu huyu, kama vile kitasa cha Mlango,n.k

-Kuwa karibu na mtu mwenye virusi hivi huku akipiga chafya za mara kwa mara

-Virusi hivi kwa asilimia kubwa hupatikana kwenye chembechembe za mate au makamasi. Vinaingia mwilini kwa kugusa au kupitia kwa kinywa, pua au macho.

JINSI YA KUJIKINGA NA CORONA AU COVID-19

(1) Mungu kwanza,Mtangulize Mungu atakulinda,kisha chukua tahadhari zingine kama;

(2) Nawa mikono kila mara baada ya kushika vifaa vyovyote,kabla ya Kula,na baada ya kutoka chooni

(3) Epuka kushika uso wako kabla ya kunawa mikono hasa ukiwa umetoka sehemu yenye msongamano wa watu wengi

(4) Kuepuka sehemu za misongamano mikubwa, kama sokoni,Bar,Club au Stend


(5) Umbali wa angalau mita 2 au futi 6 mbali na wengine,na kukaa nyumbani kama vile iwezekanavyo pia ni njia nzuri ya kuzuia kupata huu ugonjwa.

KAMA UNA TATIZO LA KWENDA HOSPTAL KUMUONA DACTARI AU MKUNGA

Utakuwa na miadi ya kuwaona madaktari na wakunga wakati unapokuwa mjamzito kwa mara kadhaa . Hizi miadi ni muhimu kwa afya yako na ya mtoto wako na unaweza kukosa kuenda hospitalini baada ya majadiliano na daktari wako au mkunga. Baadhi ya matembezi yanaweza kufanywa kwa simu au video na daktari au mkunga wako ikiwa itawezekana. utakapohisi matatizo katika ujauzito, usisite kuwasiliana na daktari au mkunga wako na ujadiliane nao njia bora ya kupata huduma. Unapotembelea  kliniki au hospitali, nawa mikono yako kila mara unapogusa vifaa, epuka kugusa uso wako kwa mikono yako na jaribu kuzingatia angalau umbali wa mita 2 au futi 6 mbali na watu wengine katika eneo la kusubiri. Lazima pia unawe mikono yako wakati unapoondoka. Ikiwa una kikohozi, Vaa barakoa mara tu unapowasili hospitalini au kliniki na ujulishe mtu mara moja kabla ya kufika ili waweze kutarajia na kujiandaa vyema kukuhudumia. Kama ukona ugonjwa wa COVID-19 na ni nafasi yako ya miadi ya kawaida, wasiliana na daktari wako au mkunga ili kuona kama ni bora kuhahirisha miadi yako kwa tarehe ingine.

 

? SASA TUZUNGUMZIE MAAMBUKIZI YA CORONA NA UJAUZITO

Japo kuwa ukiwa Mjamzito kinga yako ya mwili hushuka sana yaani unakuwa na LOW IMMUNITY lakini pia Kuna visa vichche sana vya Maambukizi ya COVID-19 kwa Wajawazito ikilinganishwa na wanawake wa umri sawa na hao ambao hawana ujauzito.

JAPO, Wanawake ambao wana matatizo mengine ya kiafya kama vile matatizo ya mapafu, shinikizo la damu, kisukari au virusi vya Ukimwi wako katika hatari kubwa ya kuugua ugonjwa wa COVID-19 ikilinganishwa na hao wengine. Kwahyo basi kuhudumiwa kwao na kuangaliwa kwao ni tofauti na hawa wengine, umakini na jicho la tatu huwatazama zaidi kuliko wanawake wengine wajawazito. Idadi kubwa ya wanawake wajawazito wenye afya zuri wanaopatikana na maambukizi ya COVID-19, watapata huduma ya afya wakiwa nyumbani, lakini wanapaswa kuonekana kwa haraka kama dalili zita badilika kuwa mbaya zaidi. Huduma ya dharura kwa wanaodhoofika ni njia bora ya kuzuia matatizo makubwa kwa mama au hujauzito. Madaktari watawapokea na kuwapa huduma stahiki kama watu wengine.Akina mama ambao wanakuwa wagonjwa sana na wanahitaji kuwa hospitalini wako katika hatari kubwa ya kwenda katika leba na wanapaswa kuangaliwa kwa makini sana.Dawa salama kwa Ujauzito kama Acetaminophen au paracetamol huweza kutumik kama mjamzito ana homa.

ATHARI ZA COVID-19 KWA MTOTO ALIYETUMBONI

Hakuna utafiti wa moja kwa moja kwamba Virusi hivi vya Corona huweza kutoka kwa mama mjamzito mwenye maambukizi haya na kupenya hadi kwa mtoto tumboni kupitia Umbilical cord na kumletea shida yoyote. Japo kuna utafiti unasema,vipimo na uchunguzi wa damu kwa watoto 3 unaonyesha kwamba kuna uwezekano walipata virusi wakati wa ujauzito. Hakuna tafiti yoyote ambayo imeonyesha kwamba COVID-19 huweza kuleta madhara kwa mtoto tumboni hasa katika swala nzima la uumbaji wake, japo kuna taarifa tu kwamba wanawake wachache ambao walikuwa na virusi wakiwa wajawazito na kisha wakapata watoto wao. Homa kali katika ujauzito ukiwa na wiki 6 au majuma 4 baada ya kupata ujauzito inaweza kuhusishwa na athari kuu ya matatizo ya uti wa mgongo na ubongo. Hii si kwa sababu ya COVID-19 mbali inaweza kuwa sababu yoyote ya kuwa na homa. Hatari inabaki kuwa ya chini sana. Takriban wanawake wawili kwa kila elfu moja,wanawake wenye homa katika ujauzito mchanga wanaweza kuzaa watoto wenye matatizo hayo ikilinganishwa na mwanamke mmoja kwa elfu moja ya kila wanawake wajawazito wenye mimba ambao hawakuwa na homa katika ujauzito mchaga. Utafiti wa picha ya ultrasound kwa ujauzito wa wiki kumi na nane hadi ishirini na mbili, unapendekezwa kulenga baadhi ya matatizo haya.

CR: @Isuog.org ?

Hatari kuu kwa mtoto ni kwamba wewe kuugua zaidi na kwenda katika leba  kabla ya tarehe yako ya kujifungua kufika au madaktari na wakunga wapendekeze kujifungua mapema kwa sababu mtoto hakui vizuri kutokana na jinsi ulivyo mgonjwa. Jinsi siku za kujifungua zinapokaribia ndivyo hatari kwa mtoto zinapungua. Ikiwa una virusi vya COVID-19 na unaenda katika leba, mwili wako unaweza kukosa uwezo wa kuchukua oksijeni sana kama ingekuwa kawaida. Hii inaweza kuifanya iwe vigumu zaidi kwa mtoto kuweza kustahimili katika leba. Imependekezwa, ikiwezekana, kujifungua katika hospitali ambapo mtoto anaweza kuangaliwa kwa karibu ama mahali huduma ya upasuaji inapatikana badala ya kujifungua kawaida, pengine tu kuwe na sababu nyingine wakati mama ana ugonjwa wa COVID-19. Kulingana na habari hafifu tulizo nazo, watoto wengine huonyesha dalili za kuathirika siku chache baada ya kuzaliwa kwa akina mama walio na ugonjwa wa COVID-19 katika wakati wa kuzaa. Inaonekana karibu kila mmoja kati ya watoto 20 wataonyesha dalili za maambukizi ndani ya siku chache za kuzaliwa. Hii inawezekana sana kwamba walipata maambukizi wakati wa kuzaa. Tunafahamu takribani watoto 3 ambao walihitaji matibabu lakini wanaonekana kuwa walipona vizuri kutokana na maambukizi ya COVID-19.

Baadhi ya tafiti za virusi sawia na COVID-19 zinapendekeza kuwa mtoto anaweza kukua pia baada ya maambukizi sawa na COVID-19. Wataalamu wengi hupendekeza angalau uchunguzi wa picha ya ultrasound wiki 2 mpaka 4 baada ya mwisho wa maambukizi ya kuhakikisha mtoto anakua vizuri. Vile vile inapendekeza kwamba uchunguzi wa picha ya ultrasound kuendelea kufanyika angalau kila baada ya wiki 4 katika ujauzito ili kuangalia jinsi mtoto anavyoendelea kukua.

Je, ni hatari kwa mtoto wangu kama nitapata COVID-19 mara tu baada ya kujifungua?

Haijulikani ikiwa akina mama wenye COVID-19 wanapaswa kutenganishwa au kutotenganishwa na watoto wao. Maeneo tofauti watachukua hatua mbali mbali kulingana na uwezo wa eneo hilo na hali ya eneo hilo kuhusu COVID-19. Mara kwa mara yapendekeza kukaa na mtoto wako kama wewe uko katika hali zuri. Hali zingine zinaweza kuhitaji ukatenganishwa na mtoto wako. Unafaa kuuliza daktari au mkunga wako ikiwa hii ndiyo hali. Unapaswa kuwa makini kuepuka kumuambukiza mtoto wako. Hii ni bora kufanyika kwa kuosha mikono yako kabla ya kugusa mtoto, kuepuka kugusa uso wa mtoto, kuepuka kukohoa au kupiga chafya juu ya mtoto au kuvaa barokoa wakati wa kumtunza mtoto wako. Wakati haumtunzi mtoto (mtoto amelala kwa mfano), jaribu kubaki angalau mita 2 au futi 6 mbali na mtoto ili kupunguza hatari ya maambukizi kwa mtoto.

Je, naweza nyonyesha kama nina COVID-19?

Baada ya kupimwa kwa maziwa ya akina mama wachache walioambukizwa na virusi, hakuna dalili ya virusi ilipatikana katika maziwa. Kumaanisha, inaonekana salama kumnyonyesha mtoto wako hata kama una maambukizi ya COVID-19. Unapaswa kuwa makini kuepuka kumuambukiza mtoto wako virusi. Hii ufanyika vyema kwa kuosha mikono yako kabla ya kugusa mtoto, kuepuka kugusa uso wa mtoto, kuepuka kukohoa au kupiga Chofya juu ya mtoto au kuvaa barokoa (mask) wakati wa kunyonyesha. Njia nyingine bora ni kutumia pampu au kukamua kwa mkono maziwa ya mama na kumpa mtu ambaye si mgonjwa kulisha mtoto. Kama wewe utapampu au kukamua maziwa kwa mkono wako, hakikisha kunawa mikono yako kabla ya kufanya hivyo.


Je, itakuwa vipi kama mtu katika ndani ya nyumba ana dalili za COVID-19 baada ya mtoto wangu kuzaliwa?

Kama wao wanashiriki sana katika utunzaji wa mtoto, wanapaswa kuwa makini ili kuepuka kumuambukiza mtoto virusi. Hii inawezakana kwa kuzingatia yafuatayo: kwa kuosha mikono yao kabla ya kugusa mtoto, kuepuka kukohoa au kupiga Chafya juu ya mtoto au kuvaa barakoa wakati wanapo mtunza mtoto.


Ikiwa hawana haja ya kuwa karibu na mtoto, ni vizuri wakae angalau mita 2 au futi 6 mbali na mtoto kila wakati. Kumbuka kunawa mikono kabla ya kumshika mtoto hata kama hujaathirika kwa kuwa unaweza kuwa ulishika vifaa katika nyumba ambavyo vina virusi vya COVID-19.  Unapaswa pia kukaa mita 2 au futi 6 mbali na watu walioathrika ili kujizuia maambukizi. Kama tayari ukona COVID-19, utafiti unaonyesha ya kwamba mwili wako utaweza kupigana na virusi mbila wewe kuugua tena. Lakini hata katika hali hii, kuosha mikono yako kabla ya kugusa mtoto wako ni njia bora ya kuzuia kubeba virusi kwa mtoto wako kutoka kwa watu mgonjwa au vifaa walivyovigusa.


Maswali unayopaswa kuuliza daktari au mkunga wako, kwa sababu miongozo hutofautiana kutoka sehemu moja ya dunia hadi nyingine:


 Nimetangamana na mtu aliye na dalili za COVID-19. Je, nafaa kupimwa?


 Nikona dalili za kuwa na COVID-19. Je, nafaa kupimwa?


Je, mimi na familia yangu tunafaa kujitega nyumbani?


 Niliathirika na COVID-19 awali nikiwa mjamzito. Ni wakati gani napaswa kufanyiwa picha ya ultrasound kwa kuangalia afya ya mtoto?


Je, ninapaswa kutenganishwa na mtoto wangu nikiwa mgonjwa?

KWA USHAURI/ELIMU/TIBA MAWASILIANO NI +255758286584 

Karibu Sana..!!


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.