Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

SARATANI YA MATITI(KANSA YA MATITI)

DALILI ZA SARATANI

SARATANI NI NINI?
 
Saratani ni hali ya ukuaji wa seli hai za mwili usio wakawaida au ulizidi kiwango,Kwahyo basi, Saratani ya matiti ni ukuaji usio wa kawaida wa seli hai zilizopo au zinazounda eneo la titi au matiti.

DALILI ZA SARATANI ZA MATITI

(1) Dalili ya awali inayoweza kutambulisha saratani ya matiti ni kuwepo kwa uvimbe kwenye titi ambao huwa na hali tofauti na sehemu nyingine za titi. 

Hata hivyo, si kila uvimbe kwenye titi unaashiria uwepo wa saratani ya matiti. Uvimbe huu huwa mgumu, unaochezacheza kwenye titi, ambapo wakati mwingine unaweza kuwa na maumivu makali au kusiwe na maumivu yeyote. 

Uvimbe huu huwepo zaidi ya mzunguko mmoja wa hedhi kwa wale ambao hawajaacha kupata hedhi.

Dalili nyingine ni pamoja na

(2) Kuwepo kwa uvimbe kwenye sehemu za kwapa

(3) Sehemu ya titi kuingia ndani inayoashiria uvimbe usioonekana au usioweza kuhisiwa

(4) Mabadiliko kwenye chuchu, kama vile chuchu kuzama ndani au kuwa na nundu ndogo ndogo, chuchu kuwasha, kuhisi kama kuchoma, kidonda kwenye chuchu au chuchu kuwa na kovu ambalo huashiria saratani ya sehemu hiyo

(5) Kubadilika kwa umbo la titi, ngozi ya titi kuwa kama ganda la chungwa (peu de orange), ngozi kuwa na rangi nyekundu, na kuongezeka kwa joto kwenye titi. Dalili hizi huashiria kusambaa kwa saratani mwilini.

(6) Dalili nyingine ni chuchu kutoa maji yasiyo ya kawaida ambayo hayana rangi. Aidha wakati mwingine, chuchu hutokwa damu au majimaji yenye rangi nyingine tofauti.

 MAMBO YANAYOCHANGIA KUPATA SARATANI YA MATITI

(1) Jinsi ya kike

(2) Kuanza hedhi katika umri mdogo.

(3) Kukoma siku katika umri mkubwa

(4) Kutozaa kabisa.

(5) Kutonyonyesha kabisa au kunyonyesha kwa muda mfupi.

(6) Utumiaji mafuta mengi katika chakula.

(7) Kutokufanya mazoezi ya mara kwa mara.

(8) Unene kupita kiasi

(9) Uvutaji sigara.

(10) Utumiaji wa pombe kupita kiasi.

(11) Historia ya saratani ya matiti katika familia.

JINSI YAKUJILINDA NA SARATANI YA MATITI

Kujichunguza mwenyewe mara kwa mara kwa mara.

Uchunguzi wa kitabibu wa matiti kila mwaka.

Uchunguzi wa matiti kwa njia ya mashine ya mionzi (mara moja kwa mwaka kwa wenye miaka zaidi ya 40).

Wanawake wote wenye umri kuanzia miaka 21 wajichunguze matiti yao siku ya 5-7 baada ya kumaliza hedhi mbele ya kioo

Madhara ya saratani ya Matiti

 
– Titi kuoza na kukatwa kabsa
– Titi kuuma sana na kutoa damu au usaha kila wakati
– Mwanamke kupoteza maisha pia
– Kushindwa kabsa kunyonyesha kama mama ananyonyesha

Kumbuka

Kutokana na tafiti nyingi zilizofanywa,Hizi hapa ni kansa mbili zinazoongoza kuwatesa wanawake
 
1️⃣ KANSA YA SHINGO YA KIZAZI/KANSA YA KIZAZI
 
2️⃣ KANSA YA MATITI

?MATIBABU YA SARATANI YA MATITI

Endapo tatizo hili litakugundulika katika stage za mwanzoni kabsa,mwanamke atapata tiba na atapona kabsa.Lakini kama akachelewa na saratani hiii au kansa hii ikafika stage (iv) ni ngumu kupona.
 
Kwahyo basi kuna umuhimu sna wa Kujichunguka kila wakati na pale unapoona mabadiliko yoyote mwilin,wahi hosptal kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Lakini pia kama hujui jinsi ya kujichunguza mwenyewe titi lako utapewa elimu yote.

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.