Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DALILI ZA MINYOO JAMII YA Ascaris lumbricoides

DALILI ZA MINYOO JAMII YA Ascaris lumbricoides

Ascariasis ni maambukizi ya Minyoo ambao hujulikana kama Ascaris lumbricoides ambapo watu wengi huipata kwa kugusana na udongo ambao una minyoo hii mfano kwa watu wanaopenda kutembea bila viatu au kutoka kwenye vitu vilivyochafuliwa kama vile Maji,chakula n.k

DALILI ZA MINYOO YA Ascaris lumbricoides

Tafiti zinaonyesha watu wengi wenye maambukizi ya Minyoo yaani Ascariasis hawana dalili zozote,

Maambukizi ya kiwango cha wastani au makubwa husababisha ishara au dalili anuwai, kulingana na sehemu gani ya mwili wako imeathiriwa.

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili hizo kulingana na eneo husika;

 • Katika mapafu

 Baada ya kumeza mayai madogo yaani (microscopic eggs) ya minyoo hawa wa Ascaris lumbricoides, huanguliwa kwenye utumbo mdogo na mabuu huhamia kupitia mfumo wa damu au mfumo wa limfu kwenye mapafu.  Katika hatua hii, unaweza kupata dalili sawa na pumu au nimonia, pamoja na:

 – Kikohozi cha kudumu

 – Kupumua kwa shida

 – Kutoa sauti wakati wa kupumua maarufu kama Wheezing sound

 Baada ya kutimia siku 10 hadi 14 kwenye mapafu, mabuu husafiri kwenda kooni

 • Katika Utumbo

 Mabuu hukomaa kuwa minyoo kwenye utumbo mdogo, na minyoo hiyo kwa kawaida hukaa ndani ya utumbo hadi kufa.  Kwa mtu ambaye amepata maambukizi ya ascariasis ya wastani, huweza kupata uvimbe kwenye utumbo na unaweza kusababisha:

 – Maumivu madogo ya tumbo

 – Kichefuchefu na kutapika

– Kuhara kinyesi cha damu

 Ikiwa una idadi kubwa ya minyoo ndani ya utumbo, unaweza kuwa na:

 – Maumivu makali ya tumbo

– Uchovu wa mwili

 – Kichefuchefu na Kutapika

 – Kupungua kwa uzito wa mwili 

– au tatizo la utapiamlo

N.k

MATIBABU YA MINYOO YA Ascaris lumbricoides

Baada ya kupata maambukizi ya minyoo jamii ya Ascaris kitendo ambacho kwa kitaalam hujulikana kama Ascariasis,

Minyoo hii hutibiwa kwa dawa mbali mbali kama vile;

✓ Albendazole

✓ Mebendazole

✓ Ivermectin

N.k

Na kwa maambukizi makubwa mgonjwa huweza kufanyiwa Upasuaji

KUMBUKA: Usitumie dawa yoyote pasipo maelekzo ya wataalam wa afya.

•Soma: Madhara ya kubana Mkojo kwa Muda Mrefu

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass