Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kutoka kuwa mpishi wa Putin hadi mkuu wa jeshi la kibinafsi la Urusi

Yevgeny Prigozhin ameibuka kama mhusika mkuu katika uvamizi kamili wa Urusi dhidi ya Ukraine, akisimamia jeshi la kibinafsi la mamluki wanaoongoza mashambulizi ya Urusi katika maeneo muhimu ya vita.

Sio mgeni katika magereza ya Urusi, aliajiri maelfu ya wahalifu waliohukumiwa kutoka jela kwa ajili ya kundi lake la Wagner – bila kujali uhalifu wao ni mkubwa kiasi gani – mradi tu walikubali kupigana kwa ajili yake nchini Ukraine.

Kabla ya Urusi kuanza mzozo ambao umekuwa mbaya zaidi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia, Prigozhin alishutumiwa kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani na kupanua ushawishi wa Urusi barani Afrika.

Mtu huyu wa mwanzo mbaya alifikiaje ushawishi kama huo – na sifa ya ukatili wa kutisha?

MWANZO

Yevgeny Prigozhin anatokea St Petersburg, mji wa nyumbani wa Vladimir Putin.

Alipatikana na hatia yake ya kwanza ya uhalifu mwaka 1979, akiwa na umri wa miaka 18 tu, na akapata kifungo cha miaka miwili na nusu kwa wizi. Miaka miwili baadaye, alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela kwa wizi na wizi, tisa kati yake alitumikia kifungo.

Alipoachiliwa kutoka jela, Prigozhin alianzisha msururu wa maduka ya kuuza mbwa huko St Petersburg. Biashara ilikwenda vizuri na ndani ya miaka michache, katika miaka ya 1990 isiyo na sheria, Prigozhin aliweza kufungua migahawa ya gharama kubwa katika jiji.

Hapo ndipo alianza kutanganyika na watu wa hadhi ya juu na wenye ushawishi mkubwa mjini St Petersburg na hatimaye Urusi kwa ujumla. Moja ya migahawa yake, inayoitwa New Island, ilikuwa mashua iliyokuwa ikipanda na kushuka Mto Neva. Vladimir Putin aliipenda sana kwamba – baada ya kuwa rais – alianza kuwapeleka wageni wake wa kigeni huko. Na ndivyo huenda wawili hao walikutana mara ya kwanza.

“Vladimir Putin… aliona kwamba sikuwa na tatizo la kuhudumia kibinafsi watu mashuhuri,” Prigozhin alisema katika mahojiano. “Tulikutana alipokuja na Waziri Mkuu wa Japan Mori.”

Yoshiro Mori alitembelea St Petersburg mnamo Aprili 2000, mwanzoni mwa utawala wa Vladimir Putin.

Bw Putin alimwamini Prigozhin kiasi cha kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwenye Kisiwa kipya mnamo 2003.

Miaka kadhaa baadaye, kampuni ya upishi ya Prigozhin ya Concord ilipewa kandarasi ya kusambaza chakula kwa Kremlin, ikimpatia jina la utani “mpishi wa Putin”. Makampuni yanayohusiana na Prigozhin pia yalishinda kandarasi za upishi zenye faida kubwa kutoka kwa shule za kijeshi na zinazoendeshwa na serikali.

Wagner

Lakini ilikuwa baada ya Urusi kuvamia Ukraine mnamo 2014 ndipo ishara zilianza kuonekana kwamba Prigozhin hakuwa mfanyabiashara wa kawaida. Kampuni ya kijeshi ya kibinafsi iliyosemekana kuwa na uhusiano naye iliripotiwa kwa mara ya kwanza kupigana na vikosi vya Ukraine katika eneo la mashariki la Donbas.

Inajulikana kama Wagner- jina la ishara ya simu inayotumiwa na mmoja wa makamanda wake muhimu wa awali. Aliripotiwa kuvutiwa na Ujerumani ya Wanazi, ambayo iliidhinisha kazi za mtunzi wa Karne ya 19 kwa propaganda.

Sadga ni kuwa, “de-Nazification” au kuondoa sera ya Wanazi nchini Ukraine ni lengo kuu lililotangazwa la uvamizi kamili wa Rais Putin nchini Ukraine uliozinduliwa Februari 2022.

Kando na Ukraine, Wagner ilikuwa ikifanya kazi barani Afrika na kwingineko, akifanya kazi ambazo ziliendeleza ajenda ya Kremlin – kutoka kuuunga mkono utawala wa Bashar al-Assad nchini Syria hadi kupambana na ushawishi wa Ufaransa nchini Mali.

Baada ya muda, kikundi cha mamluki kilipata sifa ya kutisha ya ukatili.

Wanachama wa Wagner wameshutumiwa kwa kumtesa mateka wa Syria kwa kutumia nyondo, kumkata kichwa na kisha kuuchoma moto mwili wake mwaka 2017.

Mwaka uliofuata, waandishi watatu wa habari wa Urusi waliuawa walipokuwa wakichunguza uwepo wa Wagner katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mnamo 2022, Wagner alishtakiwa tena kwa kumuua mtu kwa kutumia nyundo, kwa tuhuma kwamba “amelisaliti” kundi hilo huko Ukraine. Prigozhin alielezea kanda ya video ambazo hazijathibitishwa za mauaji hayo ya kikatili kama “kifo cha mbwa”. Baada ya wabunge wa Bunge la Ulaya kutaka Wagner kutajwa kama kundi la kigaidi, alidai kuwa amewatumia wanasiasa hao kijembe kilichotapakaa damu.

Kwa miaka mingi, Prigozhin alikanusha kuwa na uhusiano wowote na Wagner na hata kuwashtaki watu ambao walipendekeza afanye hivyo. Lakini basi, mnamo Septemba 2022, alisema alikuwa ameanzisha kikundi mnamo 2014.

Marekani, EU na Uingereza zote zimeweka vikwazo dhidi ya Wagner, lakini inaruhusiwa kufanya kazi nchini Urusi, ingawa sheria inapiga marufuku shughuli za mamluki.

Taarifa ghushi

Njia nyingine ambayo Yevgeny Prigozhin alijihusisha na siasa za ulimwengu alitegemea watu wanaoendesha taarifa za upotoshaji mitandaoni, badala ya wanaume wenye bunduki.

Kwa miaka mingi, amekuwa akishutumiwa kuwa nyuma ya kile kinachojulikana kama “magenge ya wapotoshaji” au “viwanda vilivyokodishwa mitandaoni”, ambavyo vilitumia akaunti kwenye mitandao ya kijamii na tovuti kueneza maoni ya kuunga mkono-Kremlin. Juhudi kama hizo ziliongozwa na Wakala wa Utafiti wa Mtandao wa St Petersburg (IRA), unaojulikana zaidi kwa kuingilia uchaguzi wa rais wa 2016 wa Marekani.

Mkurugenzi wa zamani wa FBI Robert Mueller, ambaye aliteuliwa kuchunguza madai ya kula njama kati ya kampeni ya Donald Trump na Urusi, alihitimisha kuwa IRA ilifanya kampeni ya mitandao ya kijamii iliyobuniwa kuzua na kuzidisha mifarakano ya kisiasa na kijamii nchini Marekani. Baadaye ilibadilika na kuwa operesheni ya kumuunga mkono Bw Trump na kumdharau mpinzani wake wa uchaguzi, Hillary Clinton, ripoti ya Mueller ilisema.

Marekani iliweka vikwazo kwa IRA na Prigozhin binafsi kwa kuingilia uchaguzi wa urais wa 2016 na kisha kujaribu kuingilia uchaguzi wa katikati ya muhula wa 2018.

Ukraine ni mlengwa mwingine mkuu wa kampeni za IRA za kutoa taarifa potofu na, kulingana na Uingereza, “askari wa mtandao” wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na Prigozhin wameshambulia nchi zikiwemo Uingereza, Afrika Kusini na India.

Kama ilivyo kwa Wagner, baada ya kukana kuhusika na kuwashtaki watu ambao walipendekeza kuwa alikuwa nyuma ya viwanda vya troll na mashamba ya roboti, Prigozhin alidai mnamo Februari 2023 kwamba “ametunga, kuunda na kuendesha” IRA.

Vita vya Ukraine

Wakati huu wote Prigozhin aliepuka kujulikana, kwa kawaida akiwasiliana na vyombo vya habari kupitia taarifa zilizotolewa na kampuni yake ya upishi, Concord.

Hii ilibadilika baada ya Urusi kuzindua uvamizi wake nchini Ukraine mnamo Februari 2022. Miezi kadhaa baada ya oparesheni hiyo, ilikuwa wazi kuwa inakwama, na huduma za Prigozhin zilihitajika tena.

Baada ya kukana kwa miaka kadhaa kwamba Wagner hata haikuwepo, tarehe 27 Julai 2022 vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na Kremlin vilikiri ghafla kwamba ilikuwa ikipigana mashariki mwa Ukraine. Prigozhin pia alianza kutuma video kwenye mitandao ya kijamii – ambayo inaonekana ilirekodiwa katika sehemu zinazokaliwa na Urusi nchini Ukraine – ambapo alijivunia ushujaa wa Wagner huko. Kufikia wakati huu, hakuna kundi nyingine ya jeshi la kibinafsi duniani iliyoweza kupata vifaa vingi, pamoja na ndege za kivita, helikopta na mizinga kama wagner

Lakini hivi karibuni ikawa dhahiri kuwa uhusiano wa Prigozhin na jeshi la Urusi ulikuwa mbaya sana. Mara kwa mara alikosoa viongozi wa ngazi ya juu wa Urusi, alidai kuwa wizara ya ulinzi ilitelekeza Wagner na wakati mmoja hata akawashutumu Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na Mkuu wa Wafanyikazi Mkuu Valery Gerasimov kwa uhaini.

Baada ya maelfu ya askari wa Urusi kuuawa nchini Ukraine, Prigozhin aliruhusiwa kusajiliwatu katika magereza. Yeye binafsi alitembelea magereza mengi na kuwaahidi wahalifu waliohukumiwa kuwa wangeweza kurudi nyumbani wakiwa huru, na hukumu zao zikiondolewa, baada ya miezi sita ya kumpigania Wagner nchini Ukraine – ikiwa wangenusurika.

Katika video moja, anasikika akiwaambia wafungwa: “Je, una mtu mwingine yeyote anayeweza kukutoa katika jela hii, ikiwa una miaka 10 ya kukaa gerezani? Mungu na Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeweza, lakini kwenye sanduku la mbao. Naweza kukutoa hapa ukiwa hai. Lakini sikurudishi ukiwa hai kila wakati.”

Idara ya kijasusi ya Uingereza inakadiria kuwa karibu nusu ya wafungwa ambao Wagner amepelekwa Ukraine ama wamejeruhiwa au kuuawa.

Mahusiano ya Prigozhin na wizara ya ulinzi yalipozidi kuwa mabaya, alizuiwa kuajiri wafungwa zaidi mapema 2023.

Krimlin

Lakini kwa nini Kremlin inahitaji mtu kama Prigozhin kuendesha kampeni ya upotoshaji na kampeni za kijeshi kote duniani?

Sababu moja kuu ni ile inayoitwa “kutokubalika” – kutumia wafanyikazi wa kibinafsi inaruhusu serikali ya Urusi kukataa kuhusika katika shughuli nyeti sana.

Na kwa nini Prigozhin aliishia katika jukumu hili? Kulingana na mwandishi wa habari Ilya Zhegulev, ambaye amesoma wasifu wa Prigozhin kwa undani, kuna sababu kadhaa.

“Hakuwahi kukataa kufanya vitendo viovu. Hakuwa na chochote cha kupoteza sifa, “Zhegulev anasema.

Zamani za Prigozhin ilikuwa sababu nyingine, anaongeza. “Putin hapendi watu wenye sifa safi kabisa, kwa sababu ni wagumu kuwadhibiti. Kwa mtazamo huu, Prigozhin alikuwa mgombea bora.”

Katika mahojiano nadra mnamo 2011, Prigozhin alisema aliwahi kuandika kitabu kwa watoto ambapo mhusika mkuu “alimsaidia mfalme kuokoa ufalme wake” na kisha akafanya “kitu cha kishujaa kweli”. Prigozhin sasa anaweza kumsaidia Rais Putin kuokoa maono yake ya Urusi, lakini hadithi ya maisha yake sio hadithi ya watoto.

Source:BBC

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.