Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ugonjwa Wa Siko Seli,chanzo,dalili na Tiba

Ugonjwa Wa Siko Seli,chanzo,dalili na Tiba

Katika Makala hii tunachambua Zaidi kuhusu Dalili za Ugonjwa Wa Siko Seli,chanzo cha ugonjwa wa Siko seli pamoja na Matibabu yake.

Siko seli ni nini?

Siko seli ni ugonjwa ambao upo kwenye kundi la inherited red blood cell disorders, ugonjwa huu kwa jina lingine hujulikana kama “Seli Mundu”

kwa kawaida seli nyekundu za damu(red blood cells) huwa na umbo linalojulikana kama biconcave disks, lakini Ugonjwa wa seli mundu husababisha umbo la seli nyekundu za damu kuwa kama ‘C’ yaani C-shaped au “sickle.” na hapa ndipo jina la ugonjwa huu kuitwa Sickle cell hutokea.(tazama shape kwenye picha)

kutokana na seli nyekundu za damu kuwa na shape au umbo lisilo la kawaida,hii hupelekea seli hizo kufa mapema zaidi.

Hayo ndyo maelezo mafupi ya utangulizi kuhusu ugonjwa wa Siko Seli

Aina za Ugonjwa wa Siko Seli

Kuna aina mbali mbali za ugonjwa wa siko seli ikiwemo;

  • HbSS
  • HbSC
  • HbS beta-thalassemia
  • HbSD
  • HbSE
  • HbSO
  • HbAS n.k

Chanzo cha Ugonjwa wa Siko seli

Siko seli ni ugonjwa ambao mtoto kuzaliwa nao, ugonjwa wa Seli mundu hutokana na kurithi kwa genes mbili ambazo huleta shida,

Mtoto hupokea genes mbili,moja kutoka kwa baba,na nyingine kutoka kwa mama, ambazo husababisha(code) matatizo kwenye hemoglobin kisha kupelekea uzalishwaji wa hemoglobin zenye shida yaani abnormal hemoglobin,

Na hapo ndipo ugonjwa wa Siko seli hutokea.

Jinsi ya Kugundua ugonjwa wa Siko seli

ugonjwa wa Siko seli huweza kugundulika kwa kufanya vipimo vya damu yaani simple blood test.

Dalili za ugonjwa wa Siko seli

Dalili za ugonjwa wa Siko seli kwa Ujumla zinahusisha zile zote za Mtu ambaye kaishiwa damu au ana tatizo la ANEMIA kama vile;

– Kushindwa kupumua vizuri

– Kizunguzungu

– Maumivu ya kichwa

– Ubaridi katika viganja na miguuni

– Unjano katika macho na ngozi au jaundice

– Weupe katika viganja, na eneo la macho liitwalo conjuctiva, ulimi na midomo

– Maumivu ya tumbo

– Homa

– Maumivu ya viungo (joint pains)

– Maumivu ya kifua

– Damu katika mkojo (hematuria)

– maumivu ya mfupa

– kuziba kwa ateri kuu (CRAO)

Matibabu ya Ugonjwa wa Siko seli

Kwa mujibu wa chapisho la Vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa yaani centers for diseases control and prevention(CDC)

Tiba pekee ya ugonjwa wa Siko seli ambayo huweza kutibu kabsa tatizo hili ni;

  • bone marrow transplant
  • Au stem cell transplant.

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je, ugonjwa wa Siko seli ni nini?

Siko seli ni ugonjwa ambao upo kwenye kundi la inherited red blood cell disorders, ugonjwa huu kwa jina lingine hujulikana kama “Seli mundu”

kwa kawaida seli nyekundu za damu(red blood cells) huwa na umbo linalojulikana kama biconcave disks, lakini Ugonjwa wa seli mundu husababisha umbo la seli nyekundu za damu kuwa kama ‘C’ yaani C-shaped au “sickle.” na hapa ndipo jina la ugonjwa huu kuitwa Sickle cell hutokea.

Je, chanzo cha ugonjwa wa Siko seli ni kipi?

Siko seli ni ugonjwa ambao mtoto kuzaliwa nao, ugonjwa wa Seli mundu hutokana na kurithi kwa genes mbili ambazo huleta shida,

Mtoto hupokea genes mbili,moja kutoka kwa baba,na nyingine kutoka kwa mama, ambazo husababisha(code) matatizo kwenye hemoglobin kisha kupelekea uzalishwaji wa hemoglobin zenye shida yaani abnormal hemoglobin,

Na hapo ndipo ugonjwa wa Siko seli hutokea.

Hitimisho

Ni muhimu sana kufahamu kuhusu Dalili za ugonjwa wa siko seli ili kupata msaada kwa haraka zaidi,

Dalili za ugonjwa wa siko seli kwa Ujumla zinahusisha zile zote za Mtu ambaye kaishiwa damu au ana tatizo la ANEMIA kama vile;

– Kushindwa kupumua vizuri

– Kizunguzungu

– Maumivu ya kichwa

– Ubaridi katika viganja na miguuni

– Unjano katika macho na ngozi au jaundice

– Weupe katika viganja, na eneo la macho liitwalo conjuctiva, ulimi na midomo

– Maumivu ya tumbo

– Homa

– Maumivu ya viungo (joint pains)

– Maumivu ya kifua

– Damu katika mkojo (hematuria)

– maumivu ya mfupa

– kuziba kwa ateri kuu (CRAO)

• Soma zaidi hapa kuhusu Ugonjwa wa Sickle cell(seli mundu)

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.