Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mitindo mbalimbali ya kujamiiana inaweza kusababisha uume uliosimama kwa muda mrefu kuvunjika

Utafiti wa Madaktari wa Idara ya Magonjwa ya Mfumo wa Mkojo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa umebainisha kuwa mitindo mbalimbali ya kujamiiana inaweza kusababisha uume uliosimama kwa muda mrefu kuvunjika ukiwemo mtindo wa Mwanaume kukaliwa juu na Mwanamke mwenye uzito mkubwa.

Utafiti wa Madaktari hao umechapishwa kwenye Jarida la kimataifa la Case za Upasuaji (International Journal of Surgery Case Reports, 108(2023)108415) ambapo wameripoti kufanya upasuaji wa kuunga uume wa Kijana mwenye umri wa miaka 27 uliovunjika wakati akijamiana na Mkewe.

Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti huo, ajali ya kuvunjika uume si suala lenye kujitokeza mara kwa mara, lina uwiano wa 1 kati ya Watu 175,000.

Hata hivyo, utafiti huo unadokeza kuwa tafiti zilizofanyika katika Mataifa ya Ulaya na Marekani zimeonesha kuwa asilimia 93.3 ya ajali za uume hutokana na kujamiiana, ambacho kilikuwa chanzo cha ajali ya uume aliyoipata Kijana aliyetibiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Vilevile, ajali za kuvunjika uume kwa kujichua (Punyeto) zinashika nafasi ya pili zikiwa na asilimia 10 huku mikao ya kujamiiana kama vile Mwanamke kukalia uume inatajwa kuwa chanzo kikuu cha ajali za kuvunjika uume.

Credit:BMH&MillardAyoUPDATES

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.