Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Takribani visa 117 vya polio vimethibitishwa na 107 kugunduliwa katika sampuli ya maji machafu barani Afrika mwaka 2023

Kwa Mujibu wa Takwimu za Shirika la afya Duniani(WHO);

“Takribani visa 117 vya polio vimethibitishwa na 107 kugunduliwa katika sampuli ya maji machafu barani Afrika mwaka 2023”.

Huku kukiwa na takribani visa 117 vya polio vilivyothibitishwa na 107 kugunduliwa katika sampuli ya maji machafu hadi sasa katika Kanda ya Afrika mwaka 2023, Tume ya Udhibitishaji wa Kanda ya Afrika “The Africa Regional Certification Commission (ARCC)” imezitaka nchi na washirika wa afya kushughulikia kwa haraka mapungufu katika chanjo ya polio ili kuepusha milipuko zaidi.

ARCC, ambayo ilifanya mkutano wake wa 31 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia tarehe 3 hadi 7 Julai, pia ilitoa wito wa kuharakisha utekelezaji wa shughuli za chanjo ya ziada, huku ikizingatia changamoto katika upatikanaji wa huduma ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusiana na jinsia.

Tume hiyo ilisisitiza umuhimu wa usawa wa kijinsia katika mapambano dhidi ya polio, ikibainisha jukumu muhimu ambalo wanawake wanalo,ikiwa ni pamoja na swala la usimamizi, ufanyaji maamuzi, usambazaji wa ujumbe na ufuatiliaji wa udhibiti wa polio. ARCC pia ilizitaka nchi kufanya maandalizi thabiti na kuhakikisha kampeni za chanjo ni za ubora wa juu zaidi.

“The guidance will allow health authorities and partners to provide focused support to strengthen microplanning and social mobilization in areas with poor campaign performance, among other key areas of action“ said Professor Rose Leke, Chair of the Africa Regional Certification Commission.

Mkutano huo uliwakutanisha wawakilishi wa mamlaka za afya za kitaifa na mikoa kutoka Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Madagascar, Mali na Msumbiji ambao wamejitolea kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa na kuunganisha nguvu katika Mpango wa Kupanua upatikanaji wa Chanjo katika maeneo ambayo ni magumu kufikiwa kwa msaada wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na washirika wengine wa afya.

Waliohudhuria walizingatia kuongezeka kwa hatari ya virusi vya polio aina ya 1 Madagaska na DRC, na kuzorota kwa utoaji wa chanjo ya kawaida wakati wa janga la COVID-19.

Wasiwasi pia ulihusu maeneo yanayoendelea kuathiriwa kiusalama, hasa nchini Nigeria n.k

Tume, kwa hivyo, ilihimiza mamlaka za afya pia kupanua matumizi ya Mifumo ya Taarifa za Geospatial ili kuboresha ubora wa ufuatiliaji na kukabiliana na milipuko.

“We are looking forward to implementing the additional ARCC recommendations to guide how we can deliver on the promise of polio-free Democratic Republic of the Congo and Africa,” said Dr Serge Emmanuel Holenn, Deputy Minister of Health of the Democratic Republic of the Congo”,

Mbali na DRC, Chad, Ethiopia, Madagascar, Mali na Msumbiji pia ziliwasilisha maendeleo katika udhibiti wa polio na mafunzo waliyojifunza.

Ingawa uidhinishaji wa kutokomeza polio hutokea katika ngazi ya kikanda, nchi zote zilizo na hali ya kutokuwa na polio zinahitajika kutoa tume ya uidhinishaji wa taarifa za kila mwaka(Annual updates), hii ni ili kusaidia au kuruhusu ufuatiliaji endelevu.

ARCC ilizipongeza mamlaka za afya kwa uongozi wao katika kukabiliana na milipuko ya polio inayoendelea, kwani “hii inaonyesha dhamira ya kina na kuendelea kwa juhudi za pamoja za nchi za Afrika na mashirika washirika katika mapambano dhidi ya polio,” alisema Profesa Leke.

ARCC ni chombo huru kilichoanzishwa mwaka wa 1998 ili kusimamia hali ya uidhinishaji ya eneo la Afrika kama lisilo na virusi vya polio. Inaendelea kutathmini utegemezi wa data katika nyaraka zilizowasilishwa na Kamati za Kitaifa za Uidhinishaji ili kuhakikisha kuwa nchi zinafuata vigezo vilivyowekwa vya uidhinishaji wa kimataifa wa virusi vya polio mwitu(wild polio virus).

ARCC hukutana mara mbili kwa mwaka ili kukagua maendeleo yaliyopatikana katika Taarifa ya kila mwaka ya uidhinishaji wa nchi zilizochaguliwa kuhusu shughuli za kutokomeza polio katika nchi wanachama 47 wa kanda ya Afrika ya WHO.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.