Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ugonjwa wa kisukari na upungufu wa nguvu za kiume

Ugonjwa wa kisukari na upungufu wa nguvu za kiume

Kuwa na kiwango cha juu cha sukari kwenye damu kwa muda mrefu kunaweza kusababisha matatizo mbali mbali ikiwemo kuathiri uwezo wako wa kufanya tendo la ndoa, hali hii kwa kitaalam hujulikana kama sexual dysfunction.

Watu wengi huwa na tatizo kwenye uwezo wa kufanya tendo la ndoa wakati fulani katika maisha yao, iwe wana kisukari au la. Na kuwa na kisukari haimaanishi kuwa utakuwa na tatizo hilo moja kwa moja,

Lakini watu wenye ugonjwa wa kisukari wako katika hatari zaidi ya kupata matatizo wakati wa kujamiiana hasa tatizo hili la kupungua kwa Nguvu za Kiume.

Hii ni mojawapo ya matatizo au madhara yanayotokana na ugonjwa wa kisukari, na hutokea kwa sababu ya viwango vya juu vya sukari kwenye damu, pamoja na shinikizo la damu bila kusahau mafuta kwenye damu/lehemu au (cholesterol).

Kwanini Mtu mwenye Ugonjwa wa kisukari huwa kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la Upungufu wa nguvu za kiume?

Kuwa na kiwango cha juu cha sukari kwenye damu kwa muda kunaweza kuharibu mishipa ya damu pamoja na neva, Hapa ni pamoja na mishipa ya damu na nerves zinazosambaa kwenye uume wako,

uharibifu huu unaweza kuzuia kiasi cha damu inayotakiwa kupita kwenye viungo vyako vya Uzazi ikiwemo UUME, hivyo unaweza kupoteza hisia. Hii inaweza kumaanisha pia;kuwa na shida ya kupata msisimko, kimwili na jinsi unavyohisi.

Na hapa ndipo matatizo ya kupungua uwezo wa kufanya tendo la ndoa,kukosa hisia/hamu,uume kushindwa kusimama au Upungufu wa nguvu za Kiume huanzia.

Upungufu wa nguvu za kiume

Mojawapo ya matatizo kwenye tendo la ndoa ambayo huwapata sana wananaume ni pamoja na hili la uume kushindwa kusimama kabsa au uume kushindwa kuendelea kusimama wakati wa tendo la ndoa,kwa kitaalam huitwa “Erectile dysfunction”.

Na dalili za awali kabsa ni pamoja na–hii ya uume kushindwa kusimama kabsa wakati wa asubuhi.

Wanaume wenye ugonjwa wa Kisukari wapo kwenye hatari zaidi ya mara tatu(3) ya kupata tatizo la uume kushindwa kusimama kabsa au uume kushindwa kuendelea kusimama(trouble getting or keeping an erection).

Zipo sababu mbali mbali kwanini hii huweza kutokea kwa wagonjwa wa kisukari, na sababu mojawapo ni pamoja na;

  • Kupungua kwa kiwango cha damu kinachoenda kwenye mishipa eneo la uume
  • Uharibifu wa neva-nerve damage (neuropathy)
  • Pamoja na uharibifu wa mishipa ya damu
  • Wakati mwingine hata matumizi ya dawa, au hali ya kihisia wakati wa tendo.

Unaweza kupata matibabu ya tatizo hili kwa kutumia dawa mbali mbali ikiwemo;Viagra na Cialis, lakini ongea na wataalam wa afya kwanza,kabla ya kutumia dawa hizi, kwani zinaweza kusababisha matatizo ya moyo pamoja na matatizo mengine(ikiwemo vifo pia) kama zimetumika isivyosahihi.

Unaweza pia kufikiria juu ya matibabu mengine au ushauri nasaha ili kukusaidia kudhibiti tatizo hili la uume kushindwa kusimama erectile dysfunction.

Ugonjwa wa kisukari sio sababu pekee ya kusababisha tatizo la uume kushindwa kusimama, kwa hiyo sio kitu cha kuwa na aibu. Hii inatokea kwa karibu kila mwanaume wakati fulani wa maisha, na pia huweza kusababishwa na sababu zingine kama vile; uzee, dawa za kulevya, pombe,matatizo ya vichocheo mwilini n.k.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.