Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JINSI YA KUJICHUNGUZA MWENYEWE SARATANI YA MATITI

Jinsi ya kujichunguza mwenyewe saratani ya matiti, Ni muhimu sana kujua hasa kwa wewe mwanamke kwani asilimia kubwa ya Saratani ya Matiti huwapata wanawake,japo hata wanaume pia hupatwa na saratani hii ya matiti kama ulikuwa hulifahamu hili.

Saratani zinazoongoza kuwapata wanawake ni Saratani ya Mlango wa Kizazi yaani Cervical cancer pamoja na hii Saratani ya matiti au Breast Cancer, Ni muhimu sana kuzijua Dalili Za Saratani ya matiti(Breast cancer) ili kukusaidia wewe kugundua mapema endapo una tatizo hili,

Hizi hapa chini ni Baadhi ya Dalili na Viashiria vya Saratani ya matiti;

  • Chuchu kutoa usaha au Damu
  • Chuchu kuingia ndani zaidi kuliko kawaida
  • Titi lililoathirika kuwa kubwa zaidi kuliko lingine
  • Matiti kuwa na maumivu sana au kuwa na vidonda pamoja na michubuko
  • Kuwa ni vitu vigumu kwenye titi pamoja na kwapani mithili ya punje ya harage au mchele n.k

JINSI YA KUJICHUNGUZA MWENYEWE SARATANI YA MATITI

Hizi hapa ni baadhi ya hatua ambazo huweza kukusaidia kujua jinsi ya kujichunguza mwenyewe saratani ya Matiti(Breast Cancer);

1.Anza kwa kujitazama mwenyewe kwenye kioo huku ukiwa umesimama na kunyoosha mabega yako,pamoja na mikono yako ikiwa imeshika kiuno,

Baada ya kufanya hivi itakuwa rahisi sana kugundua ziwa au titi lenye utofauti kama vile wa Umbo,ukubwa,Rangi n.k

Ukiona titi moja lina shida ya kuwa na rangi ya tofauti na lingine kama vile nyekundu zaidi,chuchu imezama ndani, maumivu, chuchu na titi lote limevimba zaidi, kuna vidonda n.k Muone daktari

2.Hatua ya pili ni kunyanyua mikono yako yote miwili juu na kuchunguza kama ulivyofanya kwenye hatua ya mwanzoni,

huku ukizingatia kuchunguza vitu muhimu kama vile rangi ya titi,umbo,ukubwa,vidonda,maumivu makali,uvimbe n.k

3.Ukiwa bado kwenye kiyoo chunguza matiti yote mawili yanatoa kitu chochote? mfano; Usaha,Damu, Maji maji n.k

4.Baada ya hapo anza kufanya uchunguzi kwa kutumia vidole vyako vinne vya mkono huku sehemu ya mbele ya vidole ikitumika zaidi,zoezi hili unalifanya ukiwa umelala halafu umejinyoosha

5.Pitisha vidole vya mkono mmoja kwenye titi lako kwa kuzunguka kuanzia kwenye chuchu huku ukisambaa kuzunguka chuchu kwa kutoka nje zaidi, zoezi hili huendelea mpaka kwenye kwapa lako la mikono yote miwili na matiti yote mawili awamu kwa awamu,endapo unashika vitu vigumu mithili ya punje ya harage au mchele waone wataalam wa afya.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.