Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mhe.Ummy Mwalimu:Ziara ya kikazi nchini India kufuatia Mwaliko wa Waziri wa Afya nchini India

Waziri wa Afya, Mhe. @ummymwalimu leo Julai 25, 2023 ameanza ziara ya kikazi nchini India kufuatia Mwaliko wa Waziri wa Afya na Ustawi wa Familia wa India Mhe. Mansukh Mandaviya.

Katika siku yake ya kwanza ya ziara yake nchini India, Mhe. Ummy amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Waziri Mandivya, Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika Sekta ya Afya ikiwemo Huduma za Ubingwa Bobezi, upatikanaji wa Dawa zenye ubora na kwa bei nafuu, matumizi ya TEHAMA katika Huduma za Afya na udhibiti wa magonjwa yasiyoambukiza.

Katika ziara yake, Waziri Ummy ameongozana na watendaji ndani ya Sekta ya Afya wakiwemo, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya Prof. Pascal Rugajjo, Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi, Mkurugenzi wa Mamlaka wa Dawa na Vifaatiba TMDA Bw. Adam Fimbo pamoja na watumishi wengine ndani ya Sekta ya Afya.

via@wizara_afyatz

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.