Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Presha ya Macho, Uwezo wa Kusoma Maandishi Changamoto Mbeya

Agosti 6, 2023 Nanenane Mbeya Imeelezwa kuwa asilimia kubwa ya wananchi waliyojitokeza kupokea huduma za Uchunguzi wa Macho katika Banda la Hospitali ya Benjamin Mkapa wanamatatizo ya Presha ya Macho na Kushindwa kuona vizuri maandishi.

Hayo yamesemwana Daktari bingwa wa Magonjwa ya Macho Dkt. Joshua Yauze mapema leo akitoa tathimini ya huduma ya Uchunguzi na Matibabu ya Macho inayotolewa na Hospitali ya Benjamin Mkapa katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane Jijini Mbeya.

“Kati ya wagonjwa niliyowaona na kuwafanyia uchunguzi wengi wao wanasumbuliwa na Presha ya Macho, Kukosa uwezo wa kusoma maandishi madogo na Mtoto jicho” alisema Dkt. Youze.

Kwa mujibu wa Dkt. Joshua wagonjwa waliyopatikana na matatizo hayo wamepewa rufaa za kupewa matibabu katika Hospitali mbalimbali zilizo Jirani na mazingira wanayoishi.

Kwa upande wao wananchi waliyopokea huduma za Uchunguzi na Matibabu katika Banda la Hospitali ya Benjamin Mkapa wameishikuru kuwasogezewa huduma huku wakionesha kuridhishwa na huduma walizopokea.

“Nashukuru kwa Huduma nzuri niliyopata katika banda lenu na kwa ushauri mzuri kutoka kwa madaktari wenu nimefarijika sana,” alieleza Aisha Salum, mmoja miongoni mwa wanufaika wa huduma hizo.

Hospitali ya Benjamin Mkapa inaendelea kutoa Huduma za Uchunguzi na Matibabu katika viwanja wa John Mwakalinga yanakofanyika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane hadi yatakapo tamatishwa Agosti 8, 2023.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.