Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Wizara ya Afya yapokea nakala ya barua iliyoandikwa na wawakilishi wa madaktari waliohitimu mafunzo ya utarajali (Interns)

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema wizara hiyo imepokea nakala ya barua ya wazi ya Julai 21, 2023 iliyoandikwa na wawakilishi wa madaktari waliohitimu mafunzo ya utarajali (Interns), iliyoelekezwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa imeainisha hoja kadhaa zinazohusu malalamiko juu ya mitihani ya usajili kabla na baada ya utarajali inayotolewa na Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT).

Amesema kufuatia malalamiko hayo, ameunda Kamati huru ya uchunguzi yenye Wajumbe 13 ikiongozwa na
Mganga Mkuu wa Serikali Mstaafu
Profesa Muhammad Bakari ambayo itafanya kazi kwa kipindi cha mwezi mmoja na kufuata hadidu za rejea zilizoainishwa na wizara ya Afya ili kuchunguza msingi wa malalamiko yaliyotolewa na Madaktari tarajali hao.

Waziri Ummy amesema Kamati hiyo itatoa mapendekezo yatakayosaidia kutatuliwa kwa changamoto zitakazobainika.

“Katika muda wote ambao Kamati itakuwa inatekeleza majukumu yake, taratibu nyingine za mafunzo ya watarajali zitakuwa zinaendelea kama ilivyoainishwa kwenye sheria, Watarajali wenye changamoto tofauti na hii au inayoendana na hii tunawashauri wawasilishe changamoto hizo kwa Baraza la Madaktari ili kupata msaada zaidi,” amesema Waziri Ummy.

Amewasihi Madaktari tarajali kuwa na subira katika kipindi ambacho Kamati itakua inafanya uchunguzi na pale watakapohitajika kutoa maelezo mbele ya Kamati.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.