Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Dalili za Ugonjwa Sugu wa Kubanwa Njia ya Hewa

Dalili za Ugonjwa Sugu wa Kubanwa Njia ya Hewa.

Ugonjwa Sugu wa Kubanwa Njia ya Hewa huathiri watu wenye umri zaidi ya miaka 40, ambao wamevuta sigara kwa miaka zaidi 20. Kawaida yake unakua taratibu na baadhi ya watu wanaweza wasifahamu kuwa wana ugonjwa huu.

Ugonjwa huu huwa na dalili mbali mbali ikiwemo:

✓ Kikohozi sugu chenye makohozi:

✓ Makohozi hutengenezwa mara kwa mara.

✓ Tatizo sugu la kukosa pumzi linaloendelea kuwa kubwa linalozidishwa na mazoezi na lisilo na vipindi vya unafuu.

✓ Kuchoka mwili.

✓ Maambukizi ya kifua yanayojitokeza mara kwa mara n.k.

MUHIMU:

*Watu wenye ugonjwa sugu wa kubanwa njia ya hewa wanalazimika KUACHA kuvuta sigara. Hii ndiyo njia bora zaidi ya kupunguza uharibifu wa mapafu.

*Dawa zinaweza kutumika kupanua njia ya hewa, kupunguza hali ya muwako kwenye mapafu au kutibu maambukizi yanayoweza kusababisha muwako.

*Watu walioathirika wanaweza kusaidiwa kwa:

  • Kuepuka hewa ya baridi sana.
  • Kuhakikisha hakuna anayevuta sigara nyumbani.
  • Kupunguza uchafuzi wa hewa kwa kuondoa moshi wa mekoni na vitu vinavyoweza kuwasha/kukera.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.