Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Neymar kulipwa mara sita ya pesa alizopata PSG

Neymar kulipwa mara sita ya pesa alizopata PSG huku klabu hiyo ya Ufaransa ikikubali kumuuza kwa £77m kwa klabu ya Saudia Al-Hilal.

Paris St-Germain wamekubali mkataba wa kumuuza mshambuliaji wa Brazil Neymar kwa klabu ya Saudi Pro League Al-Hilal kwa takriban euro 90m (£77.6m) pamoja na nyongeza.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye anatazamiwa kusaini mkataba wa miaka miwili, anafanyiwa vipimo vya afya leo na anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake ndani ya saa 48 zijazo.

Uhamisho huo unategemea Neymar mwenye umri wa miaka 31 kukamilisha uchunguzi wa matibabu na makaratasi yote muhimu.

Neymar, ambaye alijiunga na PSG kwa ada ya rekodi ya dunia ya euro 222m mwaka wa 2017, aliachwa nje ya kikosi kwa sare ya Ligue 1 dhidi ya Lorient Jumamosi.

Hakuwa sehemu ya mipango ya kocha Luis Enrique kwa msimu mpya.

Neymar alifahamika kuwa analipwa euro 25m (£21.6m) kila mwaka kwa upande wa Ufaransa.

Inasemekana atalipwa euro 150m (£129.2m) kwa mwaka nchini Saudi Arabia – mara sita ya kiasi alichopata PSG.

Mbrazil huyo aliichezea PSG mechi 173, na kuisaidia klabu hiyo kushinda mataji 13, yakiwemo mataji matano ya Ligue 1, na kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa 2020.

Hata hivyo, muda wake katika mji mkuu wa Ufaransa pia umetatizwa na majeraha kadhaa ya kifundo cha mguu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona alifanyiwa upasuaji mwezi Machi ambao ulimfanya kukosa msimu uliosalia na alianza mazoezi tu Julai.

Alikosa mechi mbili za Brazil kwenye Kombe la Dunia la 2022 baada ya kuumia kwenye mechi yao ya ufunguzi ya kundi.

Mshambulizi huyo pia alikosa michuano ya Copa America ya 2019 baada ya kupasuka mishipa kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia na kuwa nje kwa wiki kadhaa mnamo 2021 kutokana na jeraha kama hilo.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.