Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA DERMATOMYOSITIS(DM) NA TIBA YAKE

TATIZO LA DERMATOMYOSITIS(DM),CHANZO NA TIBA

Hili ni tatizo linalohusisha ngozi pamoja na kudhoofika kwa misuli ya mwili, tatizo hili huwapata sana watu wenye umri kati ya miaka 40 na 60, pamoja na watoto wenye umri kati ya miaka 5 na 15, Pia tafiti zinaonyesha kwamba Wanawake huathiriwa zaidi na tatizo hili kuliko Wanaume.

DALILI ZA TATIZO LA DERMATOMYOSITIS(DM)

Tatizo hili huweza kuanza kwa gafla au kuanza taratibu na mgonjwa kupata dalili moja hadi nyingine,baadhi ya dalili hizo ni pamoja na;

– Ngozi kubadilika rangi na kuwa na rashes, baadhi ya rangi hizo ni pamoja na Violet,dusky red rashes n.k,

Hii hutokea sana kwenye maeneo kama vile usoni,kwenye viwiko vya mkono,magoti,kifua,mgongo n.k

Mgonjwa huweza kuwashwa ngozi pamoja na kupata maumivu makali

– Misuli ya mwili kulegea,Misuli ya mwili kuwa dhaifu hasa kwenye maeneo kama vile; Kwenye hips,mapaja,mabega,misuli ya mikono,shingoni n.k

CHANZO CHA TATIZO LA DERMATOMYOSITIS(DM)

– Sababu halisi au chanzo halisi hakijajulikana mpaka leo, ila kuna baadhi ya sababu ambazo zimeonekana kuongeza uwezekano wa mtu kupatwa na shida hii kama vile;

– Autoimmune disorders,

– Swala la kigenetics au vinasaba

– Matumizi ya baadhi ya dawa

– Uvutaji wa sigara

– Maambukizi ya virus yaani Viral Infection

– Swala la mazingira kama vile kukaa kwenye mionzi yajua kwa muda mrefu n.k

MADHARA YA TATIZO LA DERMATOMYOSITIS(DM)

• Mtu kupata shida ya kumeza kitu chochote

• Mtu kukosa pumzi au kushindwa kupumua

• Mtu kupatwa na shida ya pneumonia yaani Aspiration Pneumonia

Hii mara nyingi hutokea wakati chakula,kimimika chochote kama maji,juice n.k,Au mate kuingia kwenye mapafu yako

• Mtu kupata shida ya Calcium deposits, ambayo hutokea kwenye ngozi,misuli pamoja na Connective tissues

• Mtu kuwa katika hatari zaidi ya kupatwa na tatizo la kansa au saratani

• Mtu kuwa katika hatari zaidi ya kupatwa na tatizo la magonjwa ya mapafu

• Mtu kuwa katika hatari zaidi ya kupatwa na tatizo la magonjwa ya Moyo n.k

VIPIMO VYA TATIZO LA DERMATOMYOSITIS(DM) NI PAMOJA NA;

– Vipimo vya damu yaani Blood analysis

– Chest X-ray

– Electromyography

– MRI

– Skin/Muscle biopsy n.k

MATIBABU YA TATIZO LA DERMATOMYOSITIS(DM)

Hakuna tiba ya kuponya kabsa tatizo hili,ila kuna tiba ya kuboresha ngozi ya mgonjwa pamoja na misuli yake kuipa nguvu. Na hapa huhusisha;

1. Matumizi ya dawa mbali mbali jamii ya corticosteroids kama vile Prednisone

2. Matumizi ya dawa jamii ya Corticosteroids Spary agents kama vile Azathioprine,Methotrexate,Mycophenolate mofetil n.k

3. Matumizi dawa jamii ya Antimalarial medications kama vile Hydroxychloroquine kwa mtu mwenye rashes kwenye ngozi

4. Kujikinga kupigwa na jua kwenye ngozi yaani Sunexposure

5. Mgonjwa kufanyiwa upasuaji

6. Pamoja na huduma zingine kwa mgonjwa kama vile;

– Huduma ya Physiotherapy

– Huduma ya Speech therapy N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LILE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.