Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DAWA YA KUTIBU UCHAFU UNAOTOKA UKENI

Kwa asilimia kubwa ya wanawake husumbuliwa na tatizo la kutokwa na uchafu ukeni,ambapo uchafu huo huweza kuambatana na matatizo mengine kama vile miwasho sehemu za siri pamoja na harufu kali,

Uchafu huweza kutoka ukeni huku ukiwa na rangi mbali mbali kama vile; rangi ya maziwa,rangi ya manjano n.k, na kila rangi ya uchafu ni muhimu sana katika utambuzi wa aina ya ugonjwa ambao upo kwa mwanamke mwenye tatizo la kutokwa na uchafu ukeni,

Sio kila mara kwa mwanamke mwenye tatizo la kutokwa na uchafu ukeni basi awe na matatizo mengine kama vile miwasho,harufu kali,maumivu ya tumbo,maumivu wakati wa kukojoa n.k bali hutegemea na aina ya maambukizi ambayo yamempata mwanamke huyo.

Tatizo la mwanamke kutokwa na uchafu ukeni huweza kuwa ni kiashiria cha magonjwa mbali mbali kama vile; Ugonjwa wa fangasi wa ukeni maarufu kama Candida Albicans, tatizo la PID(maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya mwanamke),pamoja na magonjwa mengine ya Zinaa

UCHAFU KUTOKA UKENI HUWEZA KUAMBATANA NA MATATIZO GANI?

Kama nilivyokwisha kusema hapo awali uchafu kutoka ukeni huweza kuambatana na matatizo mengine kwa mwanamke kama vile;

– Tatizo la kupata miwasho sehemu za siri au ukeni,ikiwa ni pamoja na ngozi ya mashavu ya ukeni,eneo la katikati ya sehemu ya haja kubwa na ukeni n.k

– Kutoa harufu kali ukeni mithili ya shombo la Samaki

– Kutoa maji maji kila wakati ukiwa umevaa nguo yako ya ndani

– Kupatwa na tatizo la maumivu ya tumbo wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa

– Mwanamke kupoteza kabsa hamu ya kufanya mapenzi au tendo la ndoa N.k

DAWA YA KUTIBU UCHAFU UNAOTOKA UKENI

Matibabu ya tatizo la kutokwa na uchafu ukeni hutegemea na chanzo cha tatizo hilo,hivo baada ya kukutana na wataalam wa afya na vipimo mbali mbali kufanyika ndipo tiba huanza, Mfano;

Kama tatizo la kutokwa na uchafu ukeni chanzo chake ni ugonjwa wa Fangasi wa ukeni basi mgonjwa huanza tiba mbali mbali kama vile; Matumizi ya Clotrimazole ya vidonge vya kudumbukiza ukeni,Clotrimazole cream n.k

Kama tatizo la kutokwa na uchafu ukeni chanzo chake ni ugonjwa wa PID,basi mgonjwa huanza matibabu mbali mbali ya PID kama vile matumizi ya dawa jamii ya Doxcycline n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.