WhatsApp kuongeza viwango vya ukaguzi wa ubora dhidi ya sampuli za damu kavu (DBS) katika hospitali ya Nyerere DDH
Imeelezwa kuwa matumizi ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp yameongeza viwango vya ukaguzi wa ubora wa sampuli ya damu kavu (DBS) katika hospitali ya Nyerere DDH Mugumu Serengeti Mkoani Mara,
hali inayochangia upatikanaji wa taarifa sahihi za sampuli za damu kavu wakati utambuzi wa awali wa Virusi vya UKIMWI kwa watoto walio chini ya miezi 18 ili kujua hali zao kutokana na wazazi wao kuishi na maambukizi ya VVU.
Akizungumza Agosti 17,2023 na Waandishi wa Habari waliotembelea Hospitali ya Nyerere ambayo ni hospitali teule ya wilaya ya Serengeti, Muuguzi katika hospitali ya Nyerere DDH,
Nyanchamba Mulaga Musiba amesema uanzishwaji wa matumizi ya jukwaa la WhatsApp kama ukaguzi wa ubora wa sampuli za damu kavu ulifikiwa kwa ajili kuboresha sampuli za damu kavu na kuondoa tatizo la sampuli zinazokataliwa maabara(rejected samples).
Amesema kundi hilo la Whatsapp limeongeza ufanisi katika upimaji wa mapema wa Virusi vya UKIMWI kwa mtoto aliyezaliwa na mama mwenye maambukizi ya Virusi ya UKIMWI.