Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Twiga Adimu zaidi Duniani Azaliwa marekani

Mtoto wa twiga aliyezaliwa bila madoadoa anaweza kuwa twiga ‘adimu zaidi duniani’

Mbuga ya wanyama ya Brights iliyoko Marekani imeibua majadala mitandaoni ilipotangaza fursa ya umma kuchagua jina ambalo twiga mwenye rangi ya kipekee ya hudhurungi na asiye na madoadoa atapewa.

‘Tunayo majina 4 ya kuchagua,
1. Kipekee – Kipekee
2. Firyali – Isiyo ya Kawaida
3. Shakiri – Ni mrembo zaidi
4. Jamella – Yenye uzuri mkubwa

“Unafursa ya kuchagua hadi Septemba 4 mwaka huu.Siku hiyo, tutajumlisha kura zote na kutangaza jina la twiga huyu mdogo.”Taarifa ilisema.

Twiga huyu ni wa aina ya “reticulated”, mojawapo ya spishi nne za twiga.

Muasisi wa hifadhi hiyo ya wanyama Tony Bright alisema huyu anaweza kuwa “twiga pekee mwenye rangi moja anayeishi popote kwenye sayari.”

Neno “reticulated” linashiria madoadoa ya rangi ya hudhurungi na nyeupe yenye pembe nyingi kwenye ngozi yake.

Twiga hutumia rangi hii kujikinga dhidi ya adui kama simba na wanyama wengine ambao huwala nyikani kaskazini mwa Kenya ambapo wanaishi.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.