Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Jenerali wa Urusi ambaye aliendesha vita vya Ukraine afukuzwa kazi

Mmoja wa viongozi wakuu wa jeshi la Urusi, Jenerali Sergei Surovikin, ameripotiwa kupoteza kazi yake kama mkuu wa jeshi la wanahewa baada ya wiki kadhaa za uvumi kuhusu kutoweka kwake mbele ya watu.

Shirika la Ria Novosti lilisema kuwa ameondolewa kwenye wadhifa wake, likinukuu chanzo.

Kwa miezi kadhaa Jenerali Surovikin alikuwa akisimamia uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine lakini hajaonekana tangu maasi ya Wagner mwezi Juni.

Waangalizi wanaamini kuondolewa kwake kulianza wakati wa uasi ulioshindikana.

Ripoti moja ya Urusi ilinukuu chanzo cha wizara ya ulinzi kikisema kwamba amefukuzwa kazi kwa sababu ya uhamisho wa kazi mpya na sasa yuko likizo fupi.

Jukumu lake kama mkuu wa vikosi vya anga limechukuliwa na mkuu wa wafanyikazi wa jeshi la anga, Jenerali Viktor Afzalov, Ria Novosti anaongeza.

Wakati wa saa ambazo mamluki wa Wagner waliandamana kuelekea Moscow tarehe 24 Juni, Jenerali Surovikin alionekana kwenye video akiwaomba warudi kituoni.

Lakini utendakazi wake mbaya baadaye ulilinganishwa na video ya mtindo wa mateka. Jenerali huyo alijulikana kuwa na uhusiano mzuri na chifu wa Wagner Yevgeny Prigozhin, ambaye aliweka chuki yake kwa watu wengine katika uongozi wa ulinzi.

Wiki chache baada ya uasi wa Juni, kulikuwa na ripoti ambazo hazijathibitishwa na wanablogu wa kijeshi wa Urusi kwamba Jenerali Surovikin alikuwa amezuiliwa kwa mahojiano. Lakini maafisa walikanusha kuwa anazuiliwa katika kituo cha kizuizini cha kabla ya kesi na jenerali mmoja aliyestaafu alisema kuwa “anapumzika” tu na hapatikani.

Jenerali Surovikin, mkongwe wa miaka 56 wa kampeni ya Usovieti nchini Afghanistan katika miaka ya 1980, alipewa jina la utani Jenerali Armageddon kwa mbinu zake za kikatili nchini Syria.

Akiwa kamanda wa majeshi ya Urusi na baadaye jeshi la anga aliacha sehemu kubwa ya mji wa pili, Aleppo, ukiwa magofu na kuwashambulia raia katika jimbo linalodhibitiwa na waasi la Idlib. Alikuwa afisa wa kwanza wa jeshi kuongoza vikosi vya anga vya Urusi na hakuwa na uzoefu wa anga.

Kupandishwa cheo kwake kulikuja mnamo Oktoba 2022, alipofanywa kuwa kamanda wa vikosi vya Urusi nchini Ukrainia, miezi kadhaa baada ya uvamizi mkali na wa kiwango kikubwa.

Miezi yake mitatu ya uongozi haikufanikiwa. Siku ambayo aliteuliwa, daraja la Mlango-Bahari wa Kerch lilishambuliwa, na wiki kadhaa baadaye aliamuru kurudi kutoka kwa jiji la Kherson. Ndani ya miezi mitatu alibadilishwa na mkuu wa wafanyikazi wa Urusi Valery Gerasimov, na kuwa mmoja wa manaibu wake.

Viongozi wa kijeshi wa Urusi wamekuwa na machache ya kujivunia tangu Rais Vladimir Putin alipotuma wanajeshi mnamo Februari 2022 na viongozi wengi wa juu wamehamishwa hadi nyadhifa tofauti.

Kabla ya Jenerali Surovikin kuwekwa msimamizi wa operesheni hiyo, juhudi za vita ziliendeshwa na Kanali Gennady Zhidko. Alikufa huko Moscow wiki iliyopita baada ya kile maafisa walisema kuwa “ugonjwa wa muda mrefu”.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.