Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Nchi ya INDIA kubadilishwa jina lake na kupewa jina la ‘Bharat’

Nchi ya INDIA kubadilishwa jina lake na kupewa jina la ‘Bharat’

Serikali ya India chini ya Waziri Mkuu Narendra Modi imebadilisha jina la India na kuipa Nchi hiyo jina la ‘Bharat’ katika kadi za mialiko ya chakula cha jioni zilizotumwa kwa Wageni watakaohudhuria mkutano wa kilele cha G20 wiki hii na kuongeza uvumi kwamba jina la Nchi hiyo litabadilishwa rasmi hivi karibuni.

Rais wa India, Droupadi Murmu alijitambulisha kama “Rais wa Bharat” badala ya “Rais wa India” katika kadi hizo zilizotumwa kwa Wageni wanaohudhuria mkutano wa G20.

India ni Mwenyeji wa mkutano unaofanyika kila mwaka wa G20 likiwa ni kongamano baina ya Serikali zinazojumuisha Nchi 19 pamoja na Umoja wa Ulaya Jijini New Delhi, Viongozi wengi duniani akiwemo Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron watahudhuria.

Taifa hilo lenye zaidi ya Watu bilioni 1.4 linajulikana rasmi kwa majina mawili, India pamoja na Bharat lakini jina la India ndio linatumika zaidi ndani na nje ya Nchi hiyo. ‘Hindustan’ ni neno lingine linalotumika kuitambua Nchi hiyo na mara nyingi hutumiwa katika fasihi na aina nyingins za tamaduni maarufu nchini humo.

Mapema hii leo Vyomvo vingi vya Habari nchini India viliripoti kwamba Serikali inaweza kupeleka azimio la kubadilishwa kwa jina la nchi hiyo kutoka“India” na kuitwa “Bharat” wakati wa kikao cha Bunge maalum mwezi huu.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.