Ukraine inasema shambulizi la kombora la Ijumaa kwenye makao makuu ya meli ya Urusi lilipangwa
Ukraine inadai shambulizi la Sevastopol lilishambulia makamanda wa jeshi la wanamaji
Ukraine inasema shambulizi la kombora la Ijumaa kwenye makao makuu ya meli ya Urusi ya Bahari Nyeusi huko Crimea lilipangwa kwenda sambamba na mkutano wa maafisa wa wanamaji.
Katika taarifa fupi, jeshi la Ukraine lilidai kuwa shambulizi hilo limesababisha vifo na majeruhi lakini hawakutoa maelezo zaidi.
Siku ya Ijumaa Moscow ilisema mwanajeshi mmoja alipotea baada ya shambulizi hilo.
Meli hizo zilizoko katika mji wa bandari wa Sevastopol, zinaonekana kuwa bora zaidi kati ya za jeshi la wanamaji la Urusi.
Chanzo cha jeshi la Ukraine kiliiambia BBC kwamba shambulio la Ijumaa lilitekelezwa kwa kutumia makombora ya Storm Shadow, ambayo yanatolewa na Uingereza na Ufaransa.
Taarifa ya jeshi la Ukraine siku ya Jumamosi ilidai kuwa imewaacha “mamia ya wakaaji waliouawa na waliojeruhiwa, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa meli”.
Mkuu wa ujasusi wa Kyiv, Kyrylo Budanov, alidai kuwa makamanda wawili wa Urusi walijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo la kombora.
BBC haiwezi kuthibitisha kwa uhuru madai mengi yanayohusu uwanja wa vita yaliyotolewa na pande zote mbili.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov alisema mataifa yenye nguvu ya Magharibi “yanapigana dhidi yetu, kwa kutumia mikono na miili ya Waukraine”.