Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA GAUCHER,chanzo,dalili na Tiba(GAUCHER DISEASE)

       GAUCHER DISEASE

• • • • • •

UGONJWA WA GAUCHER,chanzo,dalili na Tiba(GAUCHER DISEASE)


Ugonjwa wa gaucher ni ugonjwa ambao huhusisha mafuta kujikusanya kwenye viungo muhimu sana vya mwili kama vile kwenye INI na Wengu(Spleen).


CHANZO CHA UGONJWA WA GAUCHER


• ugonjwa wa Gaucher hutokana na tatizo la kigenetic ambapo mtu hurithi vinasaba vya tatizo hili katika familia au koo husika (Autosomal recessive),


Mgonjwa mwenye ugonjwa huu baada ya Fatty substances kujikusanya kwa pamoja kwenye viungo hivo huanza kupata dalili mbali mbali,


DALILI ZA UGONJWA WA GAUCHER NI KAMA VILE;


– Mtu kupata maumivu makali ya tumbo


– Kuwa na shida kwenye mifupa ya mwili ikiwa ni pamoja na; kuwa na mzunguko hafifu sana wa damu kwenye mifupa, mifupa kuwa dhaifu, mifupa kuvunjika kwa haraka zaidi n.k


–  Mwili kuchoka kupita kawaida


– Kuathiriwa kwa seli ambazo huhusika na swala la damu kuganda yaani  clotting, hali ambayo hupelekea mgonjwa kuvuja damu kama vile puani n.k


– Kupungua sana kwa seli nyukundu za damu yaani RED BLOOD CELLS hali ambayo hupelekea mtu kuwa na tatizo la damu kuisha mwilini yaani ANEMIA


MADHARA YA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;


✓ kuwa na tatizo la mifupa ya mwili kuwa hafifu na kuvunjika kwa haraka zaidi


✓ Kuvuja damu bila kuganda


✓ Kuwa na tatizo la kuishiwa na damu mwilini


✓ Mtu kuchelewa kwenye hatua zake za ukuaji yaani KUBALEHE au puberty


✓ Kuwa na matatizo ya Uzazi


✓ Kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa Parkinsons


✓ Kuwa katika hatari ya kupata kansa au saratani mbali mbali kama vile; Lymphoma, Leukemia, Myeloma n.k


MATIBABU YA UGONJWA WA GAUCHER


– Ugonjwa huu huweza kuhusisha matibabu mbali mbali kama vile;


• Huduma ya Enzyme replacement therapy


• Matumizi ya Dawa mbali mbali kama vile; Cerdelga, Zavesca n.k


• Huduma ya Upasuaji

N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.