Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mtoto mwenye umri wa miaka 14 akamatwa kwa kubaka watoto wawili – Mtwara

Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamshikilia Mtoto mwenye umri wa miaka 14 ambaye ni Mkulima na Mkazi wa Kitongoji cha Chiano Kata ya Nalingu, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kwa tuhuma za kubaka na kulawiti Watoto wawili (pichani) ambao ni Ndugu (Watoto wa Dada yake) ambao alikuwa anaachwa nao nyumbani kama Mlezi pindi Dada yake anapokwenda kufanya shughuli zake za kila siku za kujiingizia kipato.

Mama Mzazi wa Watoto hao ameiambia @AyoTV_ kwamba alipomuhoji Mdogo wake amekiri kufanya hivyo ambapo amesema Mtoto wa kike amembaka hadi akazoea na sasa anamuona kama Mke wake huku Mtoto wa kiume akiwa amemuingilia kwa siku tatu na alikuwa anafanya hivyo Mama yao anapokuwa mbali na nyumbani huku akiwatishia kuwa wakimwambia Mama yao atawapiga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo amesema Mtoto aliyebakwa ni wa kike mwenye umri wa miaka saba na wa kiume wa miaka mitano amelawitiwa ambapo matukio hayo yametokea kuanzia October mosi hadi 15, mwaka huu, katika nyakati tofauti.

“Alimbaka Mtoto wa kike na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri na kisha alimlawiti Mtoto wa kiume na kumsababishia maumivu katika sehemu yake ya haja kubwa, mbinu aliyotumia Mtuhumiwa kuwafanyia vitendo hivyo Wahanga hao ni pamoja na kuwavamia nyakati za usiku wakiwa wamelalala kisha kuwaingilia mmoja baada ya mwingine, wote wawili wamefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na hali zao zinaendelea vizuri”

RPC Katembo amesema kiini cha tukio ni tamaa za kimwili hivyo ametoa rai kwa Wananchi wa Mtwara, kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia pamoja na maadili yanayokinzana na sheria za Nchi…… licha ya umri wao kuwa Mdogo Watoto hao wote watatu hawasomi Shule.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.