Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

NMB yaanza Kulipa Wakulima

Benki ya NMB @nmbtanzania imefanikisha malipo ya Wakulima wa zao la tumbaku zaidi ya 400 Mkoani Tabora ikiwa ni fidia ya hasara waliyoipata baada ya mashamba yao kuharibiwa na mvua kubwa za mawe zilizotokea mwezi January na May mwaka huu.

Malipo ya madai hayo ya Tsh.milioni 374 kwa kushirikiana na Kampuni ya bima ya UAP yamekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burhani ikiwa ni fidia kubwa zaidi kuwahi kulipwa kwa Wakulima wengi nchini kwa wakati mmoja.

Akiongea katika makabidhiano hayo Balozi Dkt. Burhani amesema kuwa ushiriki wa NMB katika kukamilisha malipo hayo kwa haraka kunaifanya kuwa zaidi ya Benki katika kulihudumia taifa ambapo inaendana na azma ya Serikali katika kuhakikisha wakulima wote nchini wana bima.

“Juhudi za kuhakikisha fidia hii inalipwa kwa haraka si tu zinafanya waathirika kuendelea na kilimo chao lakini pia zinawapa imani na bima na kuwaonesha umuhimu wa kuwa na kinga dhidi ya majanga hasa kupitia kubima na NMB”

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.