Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mwanaume mmoja aliyekuwa kwenye orodha yakurekebisha maumbile Muhimbili haonekani

Jopo madaktari limetumia jumla ya saa mbili kuwafanyia upasuaji wa kurekebisha maumbo ya wanawake wanne kwa lengo la kupunguza uzito katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, mwamaume mmoja aliyekuwa kwenye orodha hiyo hakuonekana leo, Oktoba 28, 2023, ikiwa ndiyo siku ambayo hospitali hiyo imeanza kutoa huduma hiyo kwa mara ya kwanza nchini.

Akizungumza nasi jijini Dar es Salaam baada ya zoezi hilo kufanyika, Mkuu wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali hiyo, Dk Erick Muhumba amesema kutokana na hali zao kuendelea vizuri, wanawake hao wanatarajiwa kuruhusiwa kutoka wodini kesho, Jumapili.

Hii ni mara ya kwanza kwa hospitali ya Tanzania kufanya upasuaji wa kurekebisha maumbo katika zililowahusisha madaktari wazawa zaidi ya 10 kwa daktari bingwa wa upasuaji kutoka India.

Kwa mujibu wa Dk Erick Muhumba, upasuaji huo ulichukua dakika 20 kwa kila mgongwa.

Hata hivyo, pamoja na maandalizi mengine, Hospitali hiyo ilifanikiwa kumaliza zoezi ndani ya saa mbili.

“Upasuaji umefanikiwa vizuri kabisa na wagonjwa wako wodi hao wote hali zao zinaeneelea vizuri kwa mtu mmoja … tutawaruhusu kesho,” ameongeza.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.