Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Nyumba,mifugo vyasombwa na maji, huku watu 15 wakipoteza maisha nchini Kenya

Kufuatia Mafurikio yaliyotokea kwa Sababu ya Mvua kubwa; Nyumba,mifugo vyasombwa na maji, huku watu 15 wakipoteza maisha nchini Kenya.

WATU 15 wamekufa baada ya kutokea mafuriko nchini Kenya, baadhi ya nyumba, mifugo imesombwa kutokana na kadhia hiyo, Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya limeeleza.

“Mpaka kufikia Jumapili nyumba 15,264 zilikuwa zimeharibiwa, na vifo vya watu 15, mifugo 1,067 imekufa”, shirika hilo limesema.

Msimu wa mvua kuanzia Oktoba hadi Disemba unaendelea kuleta changamoto kwa baadhi ya nchi Afrika.

Mafuriko yamesababisha takriban watu ishirini kupoteza maisha na wengine 12,000 kuyahama makazi yao katika eneo la Somali Mashariki mwa Ethiopia, serikali ya mtaa ilitangaza Jumamosi.

Somalia watu 14 wamekufa na 114,000 wamekimbia makazi yao tangu kuanza kwa msimu wa mvua, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kibinadamu (Ocha)

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.