Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Baba wawili ndugu,mmoja mwisraeli na mwingine Mpalestina wakutana baada ya binti zao wawili kufia Vitani

Bassam Aramin, Mwislamu wa Kipalestina, na Rami Elhanan, Myahudi wa Kiisraeli, walipoteza binti zao wachanga katika vita vya Mashariki ya Kati.

Wote wawili wanaishi Israeli, ambako watu wengi wangetarajia wawe kama maadui baada ya msiba huo.

Lakini badala ya kulipiza kisasi, Bassam na Rami walichagua njia tofauti: amani na urafiki.

Polisi wa Israel alimpiga risasi binti wa Bassam, Abir, na kumjeruhi vibaya akiwa na umri wa miaka 10. Binti ya Rami, Smadar, aliuawa katika shambulio la kujitoa mhanga la Hamas, akiwa na umri wa miaka 14.

Wanasema “maumivu yasiyovumilika” yamewafanya wajenge urafiki usioweza kutenganishwa kati ya “ndugu” – jinsi wanavyoita uhusiano wao.

CHANZO CHA PICHA,BASSAM ARAMIN / RAMI ELHANAN

Binti ya Bassam, Abir (kushoto) alikuwa na umri wa miaka 10 alipouawa, na binti ya Rami, Smadar (kulia), alikuwa na umri wa miaka 14 alipouawa.

“Sisi si wanyama, na tunaweza kutumia akili zetu. Na unaanza kujiuliza maswali kama haya – je, kuua mtu yeyote kutamrudisha binti yangu?” Rami alihoji.

“Hata kama utaua Wayahudi wengine wote duniani – sio tu Waisraeli – hautawahi kukutana na binti yangu tena,” alisema Bassam.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.