Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Wananchi wasimamisha Msafara wa Paul Makonda Ilemela

Wananchi, Wafanyabiashara na wadau mbalimbali Wilayani Ilemela wamesimamisha msafara wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Cde. Paul Makonda kwa kumtaka kumpa salamu zao za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utendaji kazi wake uliotukuka katika kutekeleza miradi mbalimbali Wilayani humo.

“Tunaendelea kumshukuru Rais Samia hakika ni Mama yetu kwani hakuna Mama anayeweza kumuacha mwanae, Mwanza tunaendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo tunaomba umfikishie salamu zetu, pia tunakushukuru kwa kukuleta wewe, zamani nilikuwa nimezoea kukuita Mkuu wa Mkoa lakini kwasasa naomba nikuite Mkombozi wa Chama, Msaidie Rais wetu sababu wapo baadhi ya Viongozi hawafanyi kazi ni kama wamelala tuu,” alisema mmoja katika wafanyabiashara wa stendi hiyo ya Nyamuhomongoro.

Mbali na hilo, wametoa kero na changamoto zao mbalimbali zinazowakumba katika ufanyaji wa shughuli zao za kiuchumi katika stendi hiyo ya Nyamongoro.

Mwenezi Makonda alikuwa njiani kutekea Mwanza kuelekea Mkoani Simiyu katika muendelezo wa Ziara yake, leo tarehe 13 Novemba, 2023.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.