Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la kuhisi kuchomwa kwenye njia ya Mkojo,chanzo na Tiba yake

Tatizo la kuhisi kuchomwa kwenye njia ya Mkojo,chanzo na Tiba yake

Iwe wewe ni mwanamume au mwanamke, unapohisi kuungua kwenye ncha ya urethra(njia ya mkojo) mara nyingi huwa ni ishara ya maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI) au magonjwa ya zinaa (STI) kama vile klamidia au kisonono. Hata hivyo, kunaweza kuwa na sababu nyingine.

Sababu nyingine kubwa ya tatizo hili la kuchomwa kwenye njia ya mkojo(urethra) mbali na UTI au magonjwa ya Zinaa, ni tatizo la kuvimba kwa njia ya mkojo ambapo kwa kitaalam hujulikana kama urethritis, Ingawa tatizo hili pia kuweza kusababishwa na magonjwa ya Zinaa.

Chanzo cha Tatizo la kuhisi kuchomwa kwenye njia ya Mkojo

1. Maambukizi kwenye njia ya Mkojo(UTI)

Kwa UTI, bakteria huweza kuingia kwenye kibofu cha mkojo ambapo huongezeka na kuenea kupitia mfumo wa mkojo wa mwili. Baadhi ya watu hupata UTI baada ya kujamiiana kwa njia ya mdomo, uke au njia ya haja kubwa jambo ambalo linaweza kuhatarisha urethra kuweza kushambuliwa na bakteria.

Kwa ujumla, wanawake wana uwezekano mkubwa wa kupata UTI kuliko wanaume, kwa sababu mrija wa urethra kwao ni mfupi kuliko kwa wanaume. Kwa hiyo, bakteria yoyote akiingia kwenye urethra anahitaji tu kusafiri umbali mfupi kabla ya kufikia kibofu cha mkojo, ambapo bacteria hawa wanaweza kuenea kupitia njia ya mkojo.

2. Magonjwa ya zinaa (STI);

Unaweza kupata shida ya kuhisi hali ya kuungua au kuchomwa kwenye njia ya mkojo(urethra) baada ya kuwa na magonjwa ya Zinaa,

Hapa tunazungumzia Kuwa na magonjwa ya zinaa kama vile;

  • klamidia
  • au kisonono.

3. Tatizo la mawe kwenye Figo(Kidney stones)

Mawe kwenye figo ni mkusanyiko mgumu wa madini na chumvi ambayo huundwa ndani ya figo na kupita kwenye njia ya mkojo. Mara nyingi mawe kwenye figo ni matokeo ya upungufu wa maji mwilini, lishe duni, au maambukizi. Jenetiki pia inaonekana kuwa na jukumu la iwapo mtu anapata mawe kwenye figo au la.

Wakati mwingine mawe haya hufikia ncha ya urethra wakati wa kukojoa. yanaweza kusababisha maumivu sana wakati wa kupita, hasa ikiwa ni makubwa kwa umbo. Baadhi ya mawe kwenye figo ni madogo kama sehemu ya inchi moja, na mengine yana urefu wa inchi kadhaa.

4. Tatizo la Urethral stricture

Mrija wa mkojo au urethra unaweza kupungua ukubwa wake,kubanwa, kuwa na vidonda au makovu,

Kupungua kwa urethra kunaweza kusababisha kuvimba au maambukizi ambayo husababisha hisia ya kuungua/kuwaka moto kwenye ncha yake.

Baadhi ya sababu za kuwa na kovu kwenye urethra ni pamoja na:

  • taratibu za matibabu kama vile endoscopy
  • matumizi ya muda mrefu ya catheter
  • majeraha kwa pelvis au urethra
  • tezi ya kibofu kupanuliwa/kukua au kuwa na shida ya tezi dume
  • upasuaji wa kuondoa tezi dume iiyokuwa kubwa
  • saratani kwenye urethra
  • tiba ya kibofu kwa kutumia mionzi
  • Na Mara nyingine sababu haijulikani.

5. Tatizo la kuvimba kwa tezi dume(Prostatitis)

Kwa wanaume, prostatitis, au uvimbe wa tezi dume, unaweza kusababisha kuungua au kupata maumivu kwenye ncha ya urethra.

Katika hali nyingi, sababu za prostatitis hazijulikani. Hata hivyo, baadhi ya wanaume wanaweza kuwa na tatizo la kuvimba kwa tezi dume(prostatitis) kama matokeo ya maambukizi ya bakteria au uharibifu wa Nerves katika njia ya chini ya mkojo.

6. Matibabu ya Saratani ya Tezi dume(Prostate cancer treatment)

Utafiti unaonyesha kuwa baadhi ya aina za matibabu ya saratani ya tezi dume huenda zikasababisha hisia ya kuungua ya kudumu kwenye urethra.

Katika utafiti mmoja, asilimia 16 ya waathiriwa wa saratani ya Tezi dume walipata maumivu kwenye urethra miaka mitano kufuatia matibabu yao ya mwisho. Wengi wa wale wanaume walioripoti maumivu ya urethra walikuwa wamepokea matibabu ya “brachytherapy”, ambayo hutoa mionzi moja kwa moja kwenye uvimbe.

7. Tatizo la Kuvimba kwa Njia ya Mkojo(Urethritis)

Sababu nyingine kubwa ya tatizo hili la kuchomwa kwenye njia ya mkojo(urethra) mbali na UTI au magonjwa ya Zinaa, ni tatizo la kuvimba kwa njia ya mkojo ambapo kwa kitaalam hujulikana kama urethritis. Ingawa tatizo hili pia kuweza kusababishwa na magonjwa ya Zinaa.

Urethritis

Mara nyingi kuvimba kwa njia ya mkojo(urethritis) husababishwa na magonjwa ya Zinaa ikiwemo;

  • Ugonjwa wa chlamydia
  • pamoja na Kisonono

Lakini pia kuna baadhi ya irritants huweza kusababisha shida hii ikiwemo;

– Baadhi ya deodorants

– lotions

– Sabuni

– Au dawa za kuua manii(spermicides)

Uchafu(Poor hygiene), kuumia hasa wakati wa kufanya ngono kupita kiasi(vigorous sex), kufanya punyeto/ masturbation, au baadhi ya medical procedures kama vile uwekaji wa Catheter ya Mkojo n.k.

Dalili za tatizo la Urethritis

Dalili zake ni pamoja na;

– Kutokwa na uchafu mwembamba na msafi kama kamasi au

– Kutokwa na uchafu mzito kama usaha

– Kuhisi kuungua wakati wa kukojoa

– Kushindwa kuzuia mkojo

– Kukojoa mara kwa mara

– Maumivu wakati wa kukojoa

– Muwasho kwenye tundu la mkojo

– Hisia za kuungua kwenye tundu la mkojo

Chanzo cha tatizo la urethritis

Kisababishi kikuu cha urethritis ni maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwenye mrija wa mkojo/urethra. Bakteria ambao huhusika ni kama vile;

  • Chlamydia trachomatis
  • Neisseria gonorrhoeae

Vimelea wengine wanaoweza kuchangia lakini kwa asilimia chache ni;

  • Mycoplasma genitalium
  • Trichomonas vaginalis
  • Herpes Simplex virus
  • Treponema pallidum
  • Neisseria meningitides
  • Ureaplasma urealyticum
  • Ureaplasma parvum
  • Candida species

Kuna visababishi vingine ambavyo havihusiani na maambukizi pia vinaweza kupelekea tatizo la urethritis kama vile;

– Uharibifu kwenye njia ya mkojo kutokana na kuwekewa mpira wa mkojo(catheter) au kifaa tiba kwenye njia ya mkojo au sababu zingine

– Uchokozi kwenye njia ya mkojo kutokana na;

✓ Kuingiziwa mpira wa mkojo na kukaa muda mrefu

✓ Msuguano kwenye njia ya mkojo kutokana na kuvaa nguo za kubana au shinikizo wakati wa kujamiana

✓ Kufanya kazi za kuongeza shinikizo kwenye njia ya mkojo kama vile kuendesha baiskeli

✓ Matumizi ya sabuni, poda na viuaji manii vyenye uchokozi kwenye ngozi na mrija wa mkojo

✓ Kuingia kwenye Ukomo wa hedhi kwa mwanamke na kutokuwa na kiwango cha estrogen cha kutosha n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.