Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

jinsi ya kutunza maziwa ya mama

jinsi ya kutunza maziwa ya mama

Je, una elimu ya kutosha kuhusu jinsi ya kutunza maziwa ya mama? vitu gani vya kufanya na vitu gani sio vya kufanya?.

Hizi kwa lugha nyingine tunaita “do’s and don’ts for breast milk storage”.

✓ Kabla ya kukamua maziwa ya mama au kushika maziwa, Hakikisha unanawa mikono yako kwa maji safi na Sabuni

✓ Kisha hifadhi maziwa yako kwenye vifaa Safi,

✓ Hakikisha vifaa unavyotumia kuhifadhi maziwa ya mama havijatengenezwa na kemikali kama vile bisphenol A (BPA).

✓ Pia unaweza kutumia vifaa vya plastic(plastic bags) vilivyotengenezwa maalum kwa ajili ya kuhifadhi maziwa ya mama,

✓ Usihifadhi maziwa ya mama kwenye vyombo ambavyo hutumika kwenye matumizi mengine “general household use”.

✓ Pia unashauriwa weka Label inayoonyesha tarehe ulipokamua maziwa kwenye vifaa vyako vya kuhifadhi maziwa ya mama,

Na kama ni kwenye vituo vya kulelea watoto, hakikisheni mnaweka label inayoonyesha;

  1. tarehe ya kukamua Maziwa ya mama
  2. Pamoja na jina kamili la Mtoto

✓ Maziwa ya mama yahifadhiwe sehemu ambapo kuna ubaridi mfano kwenye refrigerator au freezer.

Hifadhi maziwa kwenye jokofu mara moja. Joto la jokofu linapaswa kuwa chini ya digrii 4 Celsius (39.2 Fahrenheit).

Je, unaweza kuchanganya maziwa fresh ambayo ndyo umetoka kukamua kwenye maziwa ambayo tayari umeyahifadhi?

Hili ni swali ambalo wakina mama wengi wamekuwa wakituuliza,

Usichanganye maziwa ya zamani na Sasa kama huwezi kufuata kanuni hizi hapa Chini

Je, unaweza kuchanganya maziwa fresh ambayo ndyo umetoka kukamua kwenye maziwa ambayo tayari umeyahifadhi?

Jibu: Ni ndyo, lakini kwa kuzingatia baadhi ya vitu, Fahamu maziwa ambayo yametoka kukamulia kwa mama yanakuwa na joto(warm breast milk),

Wakati unachanganya maziwa fresh ambayo ndyo umetoka kukamua kwenye maziwa ambayo tayari umeyahifadhi, hakikisha unazingatia haya;

  • Hakikisha maziwa fresh ambayo umetoka kukamua nayo yamewekwa kwenye ubaridi yakapoa vizuri kabla ya kuchanganya na yale mengine
  • Usichanganye maziwa ya mama yenye joto(warm breast milk) kwenye yale ambayo tayari umeyahidhi kwenye ubaridi.

Je, maziwa ya mama unatakiwa kuyahifadhi kwa muda gani?

Hiyo inategemea na njia unayotumia kuhifadhi maziwa ya mama, Mfano;

(i) Kama umeweka tu maziwa ya mama kwenye chombo ndani ya chumba, hapo yamehifadhiwa kwenye joto la ndani ya nyumba(Room temperature)

  • Hakikisha unayatunza kwa muda usiozidi masaa Sita, Ingawa unashauriwa kuhifadhi kwa muda wa mpaka saa nne tu kama kuna joto.

(ii) Insulated cooler; kama umehifadhi maziwa ya mama kwenye container za baridi ambazo ndani yake umeweka barafu(ice packs)

  • Hakikisha maziwa ya mama yanahifadhiwa kwa muda wa siku moja tu

(iii) Jokofu(Refrigerator); kama umehifadhi maziwa ya mama kwenye Jokofu

  • Hapa unaweza kuhifadhi maziwa ya mama kwa muda wa mpaka siku 4, ingawa wataalam wanashauri utumie yakiwa yamehifadhiwa mpaka siku 3.

Lakini Kumbuka; Tafiti zinaonyesha kadri unavyohifadhi maziwa ya mama kwa muda mrefu, kwa njia yoyote uliyotumia, ndivyo ambavyo hupoteza virutubisho ikiwemo vitamin C kwa kiwango kikubwa sana.

jinsi ya kutunza maziwa ya mama

Summary: Vidokezo muhimu vya Kuzingatia kwenye kutunza Maziwa ya mama;

(1) Usafi wa Mikono:

Osha mikono vizuri kabla ya kushughulikia maziwa ya mama. Tumia sabuni na maji safi.

(2) Vyombo Safi:

Tumia vyombo safi vya kuhifadhia maziwa kama vile chupa za plastiki au glass zilizosafishwa vizuri.

(3) Kunyonyesha Mara kwa Mara:

Jaribu kunyonyesha mara kwa mara. Hii inahakikisha mtoto anapata maziwa safi na kuchochea uzalishaji wa maziwa zaidi.

(4) Hifadhi Haraka:

Hifadhi maziwa haraka baada ya kunyonyesha. Hii inaweza kufanyika kwa kutumia chupa maalum za kuhifadhia maziwa au kwenye chombo kingine safi.

(5) Jokofu:

Hifadhi maziwa kwenye jokofu mara moja. Joto la jokofu linapaswa kuwa chini ya digrii 4 Celsius (39.2 Fahrenheit).

(6) Hifadhi kwa Muda Mrefu:

Kama unahitaji kuhifadhi maziwa kwa muda mrefu, weka kwenye freezer. Hakikisha kuandika tarehe ya uhifadhi.

(7) Tatizo la Usafiri:

Kama unasafiri na maziwa, tumia vifaa vinavyohifadhi baridi na hakikisha maziwa hayapati joto.

(8) Maziwa Yenye Kuganda:

Ikiwa maziwa yameganda kwenye jokofu, yarudishe kwa kuyachanganya kidogo kwa kusongesha chombo.

(9) Joto la Kutumia:

tumia maziwa yenye joto la mwili, kamwe usitumie microwave.

Usichanganye Maziwa ya Zamani na Mapya:

Hakikisha kutumia maziwa kwa utaratibu wa “kwanza kuingia, kwanza kutoka” ili kuhakikisha maziwa ya zamani yanatumiwa kwanza.

Kumbuka, maziwa ya mama ni chakula bora kwa mtoto na kuzingatia kanuni hizi kunaweza kusaidia kuhakikisha maziwa yanabaki safi na yenye virutubisho kwa ajili ya mtoto wako.

Rejea za Mada;

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.