Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Moja ya Matunda ambao nashauri Watu kutumia Sana ni Pamoja na papai, Je unajua Papai huweza kuwa msaada kama unapata Choo kigumu?

Moja ya Matunda ambao nashauri Watu kutumia Sana ni Pamoja na papai, Je unajua Papai huweza kuwa msaada kama unapata Choo kigumu?

Papai ni tunda Lenye faida nyingi kwenye Mwili wa Binadamu, na hata kwenye Swala la Watu ambao hupata matatizo mbali mbali kwenye choo;

Mfano; kuwa na tatizo la Choo kigumu,kutokupata haja kubwa vizuri,maumivu n.k, tumia papai na matunda mengine kama vile Parachichi.

BAADHI YA FAIDA ZA PAPAI MWILINI
• • • • • •
1. Kuua na kuondoa mazalia ya minyoo mwilini.

2. Kusaidia Mtu mwenye shida ya vidonda vya tumbo.

3. Kuboresha mmeng’enyo wa chakula.

4. Majani yake huleta ahueni kwa wagonjwa wa saratani.

5. Kupunguza uvimbe (anti-inflammatory).

6. Kuboresha misuli na neva mwilini.

7. Kusaidia kumeng’enya protini.

8. Kuboresha kinga ya mwili.

9. Kuboresha macho.

10. Kuboresha mfumo wa hewa

11. Kusaidia kwa Watu wanaopata choo kigumu,na kwashida

SOMA ZAIDI hapa…!!!!

PAPAI NA FAIDA ZAKE KIAFYA.

Asili ya mpapai ni Amerika ya kati, ambapo kuanzia matunda,majani na utomvu wa mmea huu hutumiwa kama dawa maeneo mbalimbali duniani.

Vilevile matunda na utomvu wake yamekuwa yakitumika kutengeneza pombe na mvinyo katika baadhi ya nchi,huku wengine wakitumia mpapai kama dawa kwa mifugo na binadamu.

Wataalamu wa lishe wanaeleza kuwa wenye matatizo ya kupatwa na majipu ,uvimbe na vidonda Mara kwa Mara huwa na upungufu wa virutibisho muhimu ambavyo huweza kupatikana ndani ya papai,hivyo imegundulika watu wenye matatizo hayo wakitumia papai hupata nafuu na kupona haraka.

Pia papai husaidia kuleta nuru ya macho,kama inavyoaminika kwa karoti papai pia husaidia kupunguza madhara yatokanayo na moshi wa sigara. Hivyo wavutaji wa sigara ni vyema watumie papai kwa wingi ili kujipunguzia madhara ya moshi wa sigara.

Ni wazi kuwa papai lina utajiri wa vitamini kuliko matunda mengine kwani lina vitamin A,B,C,D na E.

Tunda la papai lina faida nyingi kwa afya ya binadamu.miongoni mwa faida hizo ni ;

>Kutibu tatizo la shida ya kusaga chakula tumboni.

>Kutibu udhaifu wa tumbo.

>Kutibu kisukari na asthma au pumu.

>Kutibu kikohozi kitokacho mapafuni.

>Kutibu kifua kikuu

>Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku.

>Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda NA sehemu palipoungua moto.

MBEGU:Mbegu zake hutibu homa.meza mbegu za papai kijiko cha chakula Mara 3.

-Mbegu za papai zilizokaushwa ndani kisha kusagwa kuwa unga zinatibu malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji,kunywa Mara 3 kwa siku 5.

MIZIZI:mizizi ya papai ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa ,lita2 na nusu kwa dak 15,yanatibu figo,bladder na kuzuia kutapika. Nusu kikombe cha chai kutwa Mara 3 siku 5.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.